Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa simu za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus, basi ni vyema kufahamu kuwa kampuni ya Samsung hapo jana imeitoa simu hiyo kwenye list ya simu ambazo zinapewa support na kampuni hiyo.
Kuanzia sasa simu hizo za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus zitakuwa hazipati masasisho update yoyote ya ulinzi kama ilivyokuwa kwa miaka minne iliyopita. Hii ina maana kuwa simu hii sasa haipo kwenye list ya simu za kununua kwa sasa.
Kama wewe ni msomaji wa Tanzania tech utakuwa unajua kuhusu makala ya kwanini usinunue simu yenye umri zaidi ya miaka minne. Kama hujasoma makala hiyo basi nakushauri ukasome makala hiyo sasa.
Kwa sasa kama unataka kujua kama simu yako ipo kwenye list ya simu ambazo Samsung wana support, unaweza kubofya link hapo chini kuona kama simu yako inapatikana kwenye list ya simu hizo.
Samsung Galaxy S8 ilizinduliwa mwaka 2017 na Kioo cha inch 5.8 chenye teknolojia ya Infinity Super AMOLED curved display ambacho kina resolution ya 2960 kwa 1440.
Kwa upande wa Processor Galaxy S8 inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 835 au Exynos 8895, pamoja na RAM ya GB 4 na uhifadhi wa ndani kati ya GB 64 au GB 128.