Sio kipindi kirefu kilichopita kampuni ya Samsung ilikua ikiita uzinduzi wa simu mpya ya Note 7 “$1 billion dollar cost project” lakini baada ya matatizo yalioikuta kampuni hiyo sasa kampuni hiyo ina hasara ya zaidi ya dollar za marekani $17 Bilioni.
Hasara hii ni faida ambayo ingepatikana kama simu za Samsung Note 7 zingefanikiwa kuingia sokoni bila kuwa na tatizo lolote, hata hivyo hayo yametokea baada ya kampuni hiyo kuamua kusimamisha rasmi utengenezaji wa simu zake hizo za Samsung Note 7 ambapo siku ya juzi kampuni hiyo ilitangaza rasmi kusimamisha utengenezaji wa simu zake hizo kutokana na kile wanachosema ni kujali usalama wa watumiaji wa simu wake.
Hata hivyo hasara ya dollar za marekani $17 Bilioni imetangazwa rasmi na tovuti ya wachamubuzi ya Reuters ambayo iliandika kuwa kampuni hiyo imepata hasara hiyo baada ya kushindwa kufikia lengo lake la kuuza zaidi ya Simu milioni 19 za Samsung Note 7. Tovuti hiyo iliendelea kuandika kuwa hasara hiyo ilikuwa kubwa zaidi pale kampuni hiyo ilipoanza kurudisha simu zake hizo kutoka kwa watumiaji mbalimbali, hata hivyo inawezekana kampuni hiyo ikapata hasara zaidi (makadirio 1.6 trillion) pale itakapo amua kuanza kuzitupa simu hizo kwani nilazima kampuni hiyo izitupe simu hizo kwa usalama (kutokana na kulipuka kwake) hivyo lazima kampuni hiyo itatumia fedha kufanya hivyo. Hata hivyo hasara kamili pamoja na matatizo mengine yanayotokana na hili yatajulikana kadri siku zinavyo kwenda. Kampuni ya Samsung kwa sasa imeamua kuelekeza nguvu zake kwenye simu za Samsung Galaxy S7 pamoja na Samsung Galaxy S8 simu ambayo inategemewa kutoka mwanzoni mwa mwaka 2017.
Ili kujua zaidi kuhusu haya na mengine kutoka kampuni ya Samsung endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech kwenye simu yako ya Android, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.