Samsung ni moja ya kampuni za simu ambayo kufikia mwaka 2018 imepanga kurudi na simu za kukunja lakini zenye teknolojia mpya kabisa na zilizo boreshwa zaidi. Moja ya simu hizo ni zilizopangwa kutolewa na Samsung ni simu mpya ya Samsung W2018.
Samsung W2018 ni simu ambayo imezinduliwa rasmi leo huko nchini china na kwa mujibu wa walio fanikiwa kuiona, simu hiyo inakuja na sifa bora pamoja na muonekano wa kipekee kabisa tofauti na una-vyofikiria. Hata hivyo simu hizi ni muendelezo wa matoleo (series) ya simu za “W” ambayo yalianza kutolewa rasmi hapo mwaka jana (2017) na kampuni hiyo.
Kwa upande wa simu hii mpya ya W2018 simu hii inasemekana kuja na kioo cha ukuwa wa inch 4.2 chenye teknolojia ya AMOLED displays Full HD huku ikiendeshwa na processor ya Snapdragon 835 inayo saidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64 au GB 256.
W2018 pia inakuja na mfumo wa AI wa Bixby ambao samsung ilitangaza sasa mfumo huo utakuwa na uwezo wa kuongea kwa kichina pengine ndio sababu simu hii imezinduliwa kwanza nchini humo.
Kwa upande wa kamera W2018 inakuja na kamera ya nyuma ya Megapixel 12 huku ikiwa na uwezo wa uwezo wa f/1.5, kwa mbele simu hii ina kuja na kamera ya Megapixel 5 yenye uwezo wa f/1.9 samsung pia inasema kwa kutumia simu utakuwa na uwezo wa kurekodi video za 4K 30 fps.
Simu hii pia inakuja na battery yenye uwezo wa 2,300 mAh ambayo inachajiwa kupitia aina mpya ya USB ya USB Type C, W2018 inakuja na mfumo wa Android wa Android Nougat 7.1.1 lakini inategemewa kupata mfumo mpya wa Android 8 Oreo. Simu hii inategemewa kuja kwa rangi nyeusi lakini pia inakuja na rangi maalum za Gold na Silver.
Kwa upande wa bei simu hii inasemekana kuwa bei ghali sana na inategemewa kuunzwa kwa kati ya Euro €2000 au dollar za marekani $2400 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 5,400,000 (bei ni kwa mujibu wa viwango nvya kubadilisha fedha hivyo inaweza kubadilika kwa Tanzania).
Je unaonaje kuhusu simu hii je bei yake na muonekano wake vinalingana, tuambie kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.
Je hii simu TZ bei gan kwanza iko au haijafika
Thaman ya simu na bei haviendani kabisa hiyo simu ni ghali sana.