Wakati tukikaribia kwenye mkutano wa CES 2019, Kampuni ya Samsung imeanza mapema kwa kutangaza ujio wa kioo kipya cha kisasa kwaajili ya kompyuta. Kioo hicho kinachoitwa Samsung Space Monitor, kimetengenezwa maalum kwaajili ya kutoshea kwenye meza ndogo au kwa mtu ambaye anapenda kupata nafasi kubwa ya meza pale anapokuwa hatumii kompyuta.
Samsung Space Monitor imetengenezwa na mkono maalum ambao huu ufungwa kwenye meza na pale unapotaka kutumia kioo hicho unaweza kuvuta kioo hicho kwa mbele na mkono huo hujikunja ili kioo hicho kiweze ku-kufikia. Vilevile mkono huo ambao pia huficha nyaya ambazo mara nyingi uchukua nafasi kubwa pale mtu anapokuwa anatumia kioo cha kompyuta.
Samsung Space Monitor inakuja kwa size mbili tofauti, kioo cha inch 27 chenye QHD resolution na kioo cha inch 34 chenye teknolojia ya 4K UHD. Kioo hicho pia kinakuja na sehemu ya HDMI pamoja na viunganishi vya USB pamoja na power cable.
Kwa sasa bado Samsung haijatangaza bei ya kioo hicho, kujua zaidi kuhusu kioo hichi endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuwa mubashara kwenye mkutano wa CES 2019.