Ni kweli kwamba unapofikiria laptop bora kwa ajili ya Game huwezi kuiwaza kampuni ya Samsung, Lakini mwaka huu 2019 ni tofauti kwa Samsung kwani kupitia mkutano wa CES 2019 Samsung imezindua laptop mpya ya Notebook Odyssey ambayo ni maalum kwa ajili ya Game.
Laptop hii mpya kutoka Samsung inakuja na sifa nzuri pamoja na Graphics nzuri kiasi cha kushindana na baadhi ya laptop za Game kutoka kampuni maarufu za Razer, Dell na Alienware. Kwa muonekano binafsi naweza kusema laptop hiyo haina mtindo mzuri lakini kwa sifa laptop hii iko vizuri sana hasa upande wa Graphics.
Kwa upande wa sifa Notebook Odyssey inakuja na Graphics mpya kutoka Nvidia RTX 2080 GPU, inayosaidiwa na processor ya 8th Gen hexacore Core i7 pamoja na RAM ya GB 16. Laptop hii inakuja na kioo chan inch 15.6 chenye resolution ya 1080p pamoja na refresh rate ya 144Hz, Notebook Odyssey pia inakuja na hard disk ya SSD yenye ukubwa wa GB 256 pamoja na hard disk ya HDD yenye uwezo wa TB 1. Kwa upande wa viunganishi, Notebook Odyssey inakuja na viunganishi vya USB-A, USB-C port pamoja na sehemu za HDMI.
Kwa sasa Samsung bado haijatangaza bei ya laptop hii lakini kwa mujibu wa tovuti mbalimbali, Laptop hii inatarajiwa kuanza kupatikana rasmi mwanzoni mwa mwezi wa pili au mwezi wa kwanza mwishoni. Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujaza bei ya laptop hii itakapo tangazwa rasmi.
Kwa habari zaidi kuhusu mkutano wa CES 2019 hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia unaweza kutembelea ukurasa wetu maalum wa CES 2019 hapa.