Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Note 7 Ndio Simu ya Bei ya Ghali Kutoka Samsung

Samsung Wanategemea Kutoa Samsung Note 7 Lakini Unaijua Bei Yake..?
NOte 7 NOte 7

Baadhi ya wanunuzi wa simu za mkononi wanaosubiri simu za Samsung Note 7 na iPhone 7plus huenda wakawa kwenye wakati mgumu kidogo hii ni kutokana na kuvuja kwa bei ya Samsung Galaxy Note 7 ambayo imeonekana kuwa ya bei ghali sana kuliko matoleo yaliyopita ya samsung Galaxy S7 na S7 edge.

Ripoti kutoka katika blog ya habari za teknolojia ya Sammobile zilisema simu hiyo itauzwa kuanzia euro €849 kwa nchini europe hii ikiwa ni tofauti ya euro €50 zaidi kwa simu ya Samsung Galaxy S7 Edge, hata hivyo Samsung imeonekana kuanza kufuatilia nyayo za iPhone kwa kuangalia zaidi wateja wa hali ya juu kuliko hapo awali. Tetesi hizo hazikusema bei ya simu hizo itakuaje kwenye nchi nyingine lakini endapo bei hiyo ikawa ndio sahihi simu hiyo itauzwa kati ya shilingi za kitanzania 2069373.49 ambayo ni sawa na 2100000 TZS kwa mujibu wa kiwango cha kubadilisha fedha leo tarehe 12-07-2016.

Advertisement

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii kwenye facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use