Watu wengi sasa wanatarajiwa kumiliki simu za smart kufuatia magulio ya simu yanayofanyika Dar es Salaam na Mwanza. Magulio haya yatawapa wateja fursa ya kununua simu kwa kulipia kidogo kidogo kupitia programu maalumu iliyowekwa na Samsung kwa kushirikiana na Tigo. Wateja wataweza kuchagua kati ya simu aina ya A04 na A04s na kulipa kuanzia 1,000/TZS kila siku kwa muda wa mwaka mmoja.
Magulio hayo yameandaliwa na kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na Samsung kuanzia Aprili 17 Mlimani City Mall (Dar) na Rock City Mall (Mwanza). Gulio hilo baadaye litazinduliwa Kibo Complex-Tegeta kuanzia Mei 4. Magulio hayo yatakamilika Mei 14, 2023 ili kuwapa wateja mwezi mzima wa kufanya manunuzi ya simu za Samsung na kufurahia zawadi zenye kusisimua na vufurushi.
Pamoja na kupata unafuu wa kulipia simu hizi, wateja pia watapata uzoefu wa simu mpya za Samsung Galaxy S23 (S23 Ultra; S23 Plus na S23) pamoja na toleo jipya la A series (A34 na A 54 5G)
Wateja watakao nunua simu mpya za A series (A34 na A54) wataweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo chupa za kishua, coffe mugs na tisheti. Promosheni hii ya Nunua Ushinde itaanza wakati wa Wiki ya Eid na itahusisha pia maduka mengine ya Samsung.
Simu hizi zina kamera bomba yenye pixel ya hali ya juu yenye uwezo mzuri wa kuchukua video na picha zinazong’aa na zenye mvuto. Kama haitoshi, simu hizi zina betri imara zenye uwezo wa kudumu na chaji kwa siku mbili mfulululizo.
Simu za Samsung A34 na A54 pamoja na simu zote za Galaxy S series zinakuja na huduma ya Samsung Care+ (care plus) inayokupa ulinzi wa kioo chako kwa mwaka mzima pamoja na warranti ya Miezi 24. Vigezo na masharti kuzingatiwa.
Kwa maelezo zaidi, wateja wanaweza kutufuailia kupitia mitandao ya kijamii @samsungtanzania (Instagram) | @SamsungTanzania (Facebook) | SamsungMobileTz (twitter) | @tigo_tanzania (Instagram)
Kuhusu Samsung Electronics Co. Ltd
Samsung inatoa hamasa duniani na kuonesha njia katika masuala ya mawazo chanya na teknolojia yenye kuleta mabadiliko. Kampuni hii inaongoza katika ulimwengu wa TV, simu za smart, mitandao, memory, LSI na LED.