Mamlaka ya udhibiti ya nchini korea kusini imetoa kibali kwa kampuni ya samsung kuanza kujaribu magari yanayo jiendesha yenyewe nchini humo, imeripoti tovuti ya thenextweb.
Katika ripoti hiyo samsung inategemea kuanza kujaribu teknolojia yake mpya kwenye magari ya aina ya Hyundai alidhibitisha msemaji wa kampuni ya samsung. Hata hivyo msemaji huyo aliongeza kuwa kampuni hiyo ina nia pekee ya kujenga mifumo na mipangilio muhimu pamoja na vifaa kwa ajili ya magari hayo na sio kutengeneza magari hayo moja kwa moja.
Juhudi hizi za kampuni ya samsung zimekuja mara baada ya samsung kukamilisha ununuzi wa hisa kwenye kampuni ya HARMAN, kampuni inayo julikana sana kwa utengenezaji wa vifaa vya ndani vya magari kama redio pamoja na teknolojia mbalimbali za magari ya kisasa. Hata hivyo kukamilika kwa hatua hiyo ndio kulifanya Samsung kupata team ya wataalamu zaidi ya 8,000 walio bobea kwenye maswala ya uhandisi wa programu (software engineers) ambao kipaji chao kikubwa ni utengenezaji wa teknolojia za kisasa za magari yanayo jiendesha yenyewe.
Kampuni hiyo inasadikiwa kuwa ina uwezo mkubwa wa kutengeneza teknolojia ya kisasa ambayo ina uwezo wa kufanya sensors mbalimbali ndani ya magari hayo kutambua hali ya barabara na vikwazo, ili kufanya magari hayo kuweza kutembea vizuri kwenye hali ya hewa yoyote.
Samsung inategemewa kuanza utengenezaji huo siku za karibuni hivyo kwenye miaka ya karibuni usishangae pale kampuni ya samsung itakapo amua kuvuka mipaka na kujikita pia kwenye utengenezaji wa magari kwani sasa wanauwezo wa kufanya hivyo kutoka na kununua kampuni maarufu ya HARMAN.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.