Ikiwa zimebaki siku chache kufunga mwaka 2016 kampuni ya Samsung na Apple ziko mbioni kutoa simu zao mpya ambazo pengine ni simu zenye maboresho kuliko simu zote ambazo zimewahi kutengenezwa na kampuni hizo.
Ili kuhakikisha kuwa inatoa simu bora Samsung imedhamiria kutengeneza simu yenye sifa bora zaidi pamoja na ubora wa hali ya juu ili kuepusha yale yaliotokea kwenye simu ya Galaxy Note 7, katika kuhakikisha inaleta simu zenye sifa hizo tetesi zimeanza kusambaa kuhusu samsung huenda ikaweka kamera ya mbele (selfie camera) yenye uwezo wa kufanya Auto Focus.
Kamera yenye Auto Focus ni kamera yenye uwezo wa kujielekeza kuchukua kitu kimoja wapo kilichoko mbele au nyuma ya kitu fulani yote hayo yanafanya manual au automatic kwa kutumia kamera hiyo. Kwa upande wa Samsung S8 simu hiyo inategemewa kuja na kamera hiyo ambayo sasa utakua na uwezo wa kuchagua ni kitu gani unataka kupiga picha kwa kutumia kamera hiyo yaani kitu kilichoko mbele au nyuma ya kitu au sura yako pale unapochukua picha.
Samsung inategemewa kutumia teknolojia ya “encoder” ambayo kamera hiyo itawekewa coil kila upande ili kusaidia kamera hiyo kusogea mbele na nyuma tofauti na ile ya nyuma ambayo hutumia teknolojia ya “Voice Coil Motor”. Hata hivyo kwa mojibu wa tovuti ya teknolojia ya BGR Samsung ilikataa kuzungumzia jambo hilo kwa kusema haiko tayari kuongelea bidhaa ambazo bado hazijaingia sokoni.
Kama unataka habari zaidi za kuhusu tetesi za simu ya Samsung Galaxy S8 endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.