Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung na Apple Kutozwa Faini kwa Kufanya Simu kuwa Slow

Simu yako ya Samsung au Apple imekuwa slow baada ya ku-update..?
Update za Samsung Update za Samsung

Hivi karibuni kampuni ya Samsung na Apple zimejikuta kwenye lawama nzito baada ya kutozwa faini na serikali ya nchini italia kwa tabia ya kampuni hizi ya kutoa update ambazo zinalenga kufanya simu kuwa slow ili kufanya wateja kununua matoleo mpya ya simu kutoka kampuni hizo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Android Police, kampuni hizo mbili zimepigwa faini ya hadi Euro milioni €5 kwa kampuni ya Samsung na mara mbili ya kiasi hicho kwa kampuni ya Apple. Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti hiyo inasemekana hayo yamekuja pale mwanzoni mwa mwezi january mwaka huu ambapo kampuni hizo ziligundulika kufanya hayo baada ya mamlaka ya nchini italia kuanza kufanya uchunguzi juu ya hilo.

Advertisement

Kupitia The Autorità Garante della Concorrenza e del Mercato (AGCM) serikali ya nchini italia ilitaka kugundua kama kampuni hizo mbili zinatuma update mbaya kwenye simu za watumiaji wa simu za zamani ili kulazimisha watumiaji kubadilisha simu na kununua matoleo mapya. Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti, Samsung ilikutwa na kosa la kufanya simu ya Galaxy Note 4 kuwa slow na kampuni ya Apple ilikutwa na hatia ya kufanya uwezo wa battery kupungua kwenye simu zake za zamani.

Kwa mujibu wa Android Police, Samsung ilitoa update za Android 6.0 Marshmallow kwaajili ya Note 4 hapo mwaka 2016, lakini kwa mujibu wa ripoti hiyo samsung ilikuwa imetoa update hizo huku ikitegemea kutoa simu mpya ya Galaxy Note 7. Ripoti hiyo inasema kuwa Samsung ili sisitiza watumiaji wa Note 4 ku-install update hizo na mara baada ya watumiaji ku-update hawaku furahishwa na matokeo ya update hizo kwani yalifanya simu hiyo ya Note 4 kuwa slow zaidi na kuisha chaji kwa haraka.

Bado kampuni ya Samsung haijajibu chochote kuhusu kutozwa faini hiyo, lakini siku za karibuni kampuni hiyo imekuwa ikituhumiwa kwa makosa kama haya ya kutuma update mbalimbali kwenye simu za zamani ili kufanya ziwe slow ili wateja wanunue matoleo mapya ya simu kutoka makampuni hayo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use