Samsung ni moja kati ya kampuni ambayo ina uza simu nyingi sana kwa mwaka hapa Afrika, mbali ya kuwa simu nyingi za sasa zinakuja na sifa nzuri, lakini pia zinakuja na vitu vingi ambavyo kama wewe ni mtumiaji wa kawaida huwezi kujua kwa urahisi.
Kuliona hilo kupitia Tanzania tech tunakuletea njia mbalimbali za kujua simu za Samsung pamoja na sehemu mbalimbali ambazo huwenda ulikuwa huzijui.
Kwa siku ya leo nimekuletea sehemu mpya kupitia programu ya Samsung Members, sehemu hii inakuwezesha kujua matatizo mbalimbali ya simu yoyote ya Samsung kwa urahisi na haraka.
Kama kwa namna yoyote simu yako inakuja bila app hii, unaweza kupakua app hii moja kwa moja kupitia soko la Play Store au kupitia Samsung Store.
App hii inafaida nyingi sana lakini kwa siku ya leo ngoja tungelee njia hii ya kuangalia matatizo ya simu kwa urahisi na haraka. Hii pia inaweza kusaidia pale unapotaka kununua simu ya Samsung kutoka kwa mtu, hii itakusaidia kupata simu yenye ubora.
Baada ya kupakua app na kuinstall kwenye simu yako, moja kwa moja fungua app hii kisha sajili simu yako ya Samsung. Baada ya hapo bofya sehemu ya Get help.
Baada ya hapo utapelekwa kwenye menu ambayo itaonyesha model ya simu yako kwa juu, kisha tafuta sehemu iliyo andikwa Diagnostics. Bofya sehemu hiyo kuanza majaribio ya simu yako moja kwa moja, sehemu hii ni bora kwa kuwa majaribio haya yanakuwa ni maalum kwa simu yako.
Kwa kuwa mimi tayari nimesha anza kufanya majaribio kwenye simu yangu na kuishia katikakti basi ndio maana una ona sehemu ya View test, kama wewe ndio mara yako ya kwanza basi utaona sehemu itakayo kuonyesha kuanza majaribio.
Kama unavyoweza kuona hapo utaweza kufanya majaribio ya kila kitu kuweza kujua matatizo ya simu yako kwa ujumla. Pia kama utapata tatizo lolote utaweza kupata suluhisho kupitia app hii ya Samsung members.
Mbali na kusaidia kupata matatizo ya simu yako, pia utaweza kupata taarifa za muhimu za update ya simu yako na lini utapata update hizo. Kama unavyo jua hivi karibuni simu nyingi za Samsung zitapokea mfumo mpya wa One UI 4.0 na Android 12 hivyo utapata taarifa zote kupitia app hii.