Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Kuzindua Simu Mpya za Galaxy S20 na Galaxy Z Flip Leo

Samsung Itazindua simu hizo leo Saa 10:00 pm kwa saa za afrika mashariki
Samsung Kuzindua Simu Mpya za Galaxy S20 na Galaxy Z Flip Leo Samsung Kuzindua Simu Mpya za Galaxy S20 na Galaxy Z Flip Leo

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye leo ndio leo kwani kampuni ya Samsung inatarajia kuzindua simu zake mpya za Samsung Galaxy S20 ikiwa pamoja na simu mpya inayojikunja ya Samsung Galaxy Z Flip.

Ikiwa yamebaki masaa machache hadi kuanza kwa tamasha la uzinduzi wa simu hizi, nimekuwekea link za mambo yote ambayo yanatarajiwa kwenye simu hizo ikiwa pamoja na sifa za awali za simu zote za ambazo zinatarajiwa kuzinduliwa siku ya leo. Basi bila kupoteza muda moja kwa moja unaweza kusoma hapo chini ili kupata kujua yote yanayo tarajiwa kwenye uzinduzi huo.

Advertisement

Samsung Kuzindua Simu Mpya za Galaxy S20 na Galaxy Z Flip Leo

Kampuni ya Samsung inategemea kuzindua simu zake mpya za Galaxy S20 pamoja na toleo jipya la simu mpya inayojikunja ambayo imepewa jina la Galaxy Z Flip, mwezi huu wa pili. Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tech na Price in Tanzania, basi lazima utakuwa umefanikiwa kuona sifa za awali za simu hizo ikiwa pamoja na muonekano unaotarajiwa kwenye simu hizo.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, Samsung Galaxy S20+ yenye 5G inategemewa kuwa moja ya simu ambazo zitazinduliwa rasmi siku hiyo, simu hiyo inategemea kuwa na kamera nne kwa nyuma ambazo zipo kwenye mtindo mpya wa kisasa wa kamera ambazo zipo kwenye mzunguko wa aina yake, kama inavyo onekana kwenye picha hizo hapo chini.

Kampuni ya Samsung ina jiandaa na uzinduzi wa simu zake za daraja la juu za Samsung Galaxy S20, pamoja na toleo la pili la simu ya kujikunja ya Galaxy Fold 2. Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, Samsung inatarajia kuja na matoleo matatu tofauti ya Galaxy S20 tofauti na kipindi cha nyuma.

Fahamu kwa undani sifa za awali za Samsung Galaxy S20 5G, simu hii ni toleo kati ya matoleo ya Galaxy S20 ambapo simu hii inategemewa kuwa na mfumo wa 5G. Tofauti kubwa iliyopo kati ya simu hii na Galaxy S20 nyingine ni kuwa hii inakuja na mfumo wa 5G.

Fahamu kwa undani sifa za awali za simu mpya inayojikunja ya Samsung Galaxy Z Flip, simu hii inategemewa kuzinduliwa leo na ni simu ya kwanza ya samsung inayojikunja kwa wima, tofauti na Samsung Galaxy Fold ambayo inajikunja kwa upana au kwa upande.

Fahamu sifa za awali za Samsung Galaxy S20 Plus 5G, kama jina la simu hii linavyosema simu hii inatarajiwa kuwa na memory zaidi, ukubwa wa ndani mkubwa zaidi ikiwa pamoja na mfumo wa 5G. Utofauti wa simu hii na Galaxy S20 za kawaida ni mkubwa hivyo hakikisha unafuatilia leo ili kujua zaidi.

Na hizo ndio baadhi tu ya stori ambazo tulikuletea kuhusu simu hizi mpya za Samsung Galaxy S20 pamoja na simu mpya ya Galaxy Z Flip. Kama unataka kujua zaidi kuhusu yote yatakayo tokea kwenye mkutano huo, hakikisha una ungana na sisi kwani tutakuwa mubashara kabisa tukikuletea uzinduzi huo moja kwa moja kupitia app na website ya Tanzania Tech.

Hakikisha unaendelea kuwa nasi kuanzia muda wa Saa nne za usiku (10:00 pm) kwa saa za afrika mashariki tutakuwa mubashara kabisa kupitia tovuti hii.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use