Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yategemea Kutoa Galaxy Tab S3 Ndani ya Mwezi Huu

Jiandae kwaajili ya tablet mpya kutoka samsung mwezi huu
Galaxy Tab S3 Galaxy Tab S3

Hivi karibuni kampuni ya Samsung imetangaza kuwa sasa iko tayari kutoa tablet yake ya Galaxy Tab S3, kampuni hiyo ya samsung ilitangaza kuwa tablet hiyo itazinduliwa kwenye mkutano wa Mobile Word Congress utakao fanyika mwishoni mwa mwezi huu february huko nchini Barcelona.

Kwa mujibu wa tetesi kutoka tovuti mbalimbali za habari za teknolojia, tablet hiyo kutoka Samsung inakuja na kioo cha ukubwa wa inch 9.7, ikiwa na damension ya 2048 x 1536. Vile vile tablet hiyo itakuja na RAM ya GB 4, ukubwa wa ndani wa GB 64 pamoja na kamera ya nyuma ya MegaPixel 12 na ya mbele MegaPixel 5.

Advertisement

Hata hivyo hivi leo kume-sambaa picha ambazo zinasemekana ndio picha halisi za tablet hiyo inayotarajiwa kutoka wiki ijayo, picha hizo zilikua zikionyesha Tablet hiyo ikiwa na mabadiliko makubwa machache kama vile kuwa na glass kwa nyuma pamoja na mabadiliko mengine madogo madogo.

Kwa sasa bado haijadhibitishwa kwamba hizi ndio picha halisi za tablet hiyo mpya kutoka samsung, lakini kuna uwezekano mkubwa wa tablet hiyo kufanana na picha hizo hapo juu.

Kwa habari zaidi kuhusu tablet ya Galaxy Tab S3 hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku na ili kuwa wakwanza kupata habari za teknolojia download sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store, pia unaweza kupata habari pamoja na maujanjua ya teknolojia kwa njia ya video kupitia channel yetu ya Tanzania tech kupitia mtandao wa Youtube.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use