Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yasitisha kwa Muda Utengenezaji wa Simu Zake za Note 7

Hii ni baada ya Samsung kuanza kuuza tena simu zake za Note 7 hivi karibuni
note-7 note-7

Kampuni maarufu ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za teknolojia ya Samsung hivi karibuni ilipata hasara kubwa baada ya simu zake za Note 7 kuanza kulipuka battery zake zikiwa mikononi mwa watumiaji wake. Kulipuka huko kulisababisha kampuni hiyo kutangazia watumiaji wake kote duniani kuacha kutumia simu hizo na kurudisha simu zote za aina hiyo (Note 7) ili kujilinda pamoja na kupisha kampuni hiyo kufanya uchunguzi zaidi wa chanzo cha kulipuka kwa simu hizo.

Baada ya Samsung kutangaza hivyo kampuni hiyo ili fanikiwa kurudisha zaidi ya simu milioni ambazo zilikua zimeuzwa kwa watu mbalimbali kote duniani. Hata hivyo baadae Samsung ilitangaza rasmi kurudisha tena sokoni Simu hizo za Note 7 kuanzia mwezi October mwaka huu ambapo hadi kufikia hapo kampuni hiyo ingekua imemaliza marekebisho ya simu hizo pamoja na uchunguzi wao. Hata hivyo zoezi hilo lilianza mapema mwezi huu na simu hizo zilianza kuuzwa tena kwa baadhi ya nchi zikiwa zinajulikana kuwa kwa sasa simu hizo ziko salama baada ya kampuni hiyo kufanya uchunguzi na kurekebisha tatizo la hapo awali la simu hizo kulipuka.

Advertisement

Lakini cha kushangaza ni kwamba ndani ya mwezi huu kulianza kusambaa tena kwa taarifa mbalimbali za simu hizo mpya (ambazo zimefanyiwa marekebisho) kuendelea kulipuka japo kua kampuni hiyo ilitangaza kuwa kwa sasa simu hizo ziko salama. Kulipuka huku kuliendelea kusababisha hasara kubwa kwa kampuni ya Samsung ikiwa pamoja na kampuni kubwa za kutoa huduma za simu za nchini marekani (AT&T na T-Mobile) kutangaza rasmi kuacha kabisa kuuza na kubadilisha simu hizo za Samsung Note 7, hadi kufikia hivi karibuni (Mwezi huu wa kumi) kumesha tokea taarifa zaidi ya Saba ya simu hizo kuendelea kulipuka.

Taarifa zinasema kuendelea kulipuka kwa simu hizi kumefanya kampuni ya samsung kusitisha kwa muda kwa utengenezaji wa simu zake hizo ili kupisha uchunguzi mkubwa kwenye matawi yake yanayo simamia usambazaji wa simu zake hizo za Samsung Note 7. (moja kati ya tawi la kampuni hiyo linapatika Vietnam ambapo ndipo usambazaji mkubwa wa Note 7 kwenda nchi mbalimbali unapofanyika). Hata hivyo Samsung haijatoa maelezo rasmi ya kuhusu hili tutaendelea kuwafaamisha pindi tu samsung itakapo toa taarifa zake rasmi juu ya jambo hili.

Taarifa Mpya 11-10-2016  –  Kampuni ya Samsung imetangaza leo rasmi kuachana kabisa na utengenezaji wa simu zake za Samsung Galaxy Note 7, kwa kufanya hivyo kampuni ya Samsung itapata hasara zaidi ya dollar za marekani $17 Bilioni.

Ili kuendelea kupata habari zote za teknolojia pindi zinapotoka endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use