Hivi karibuni kampuni ya Samsung ilionyesha simu yake inayojikunja (Samsung Flex Display Phone) kupitia mkutano wa Samsung Developer Confrence, lakini baada ya kutambulisha simu hiyo tayari tetesi zimeanza kuibuka mtandaoni zikidai kuwa simu hiyo yenye uwezo wa kuwa tablet itauzwa kwa dollar za marekani $1,770 sawa na zaidi ya Tsh milioni 4 za kitanzania.
Mbali ya tetesi hizo, Simu hiyo pia inasemekana kuwa itaonyeshwa rasmi kupitia mkutano wa MWC ambao unategemewa kufanyika hapo mwezi February mwaka 2019, huku toleo la mwisho likitegemewa kupatikana mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka 2019.
Kama inavyoweza kuonekana hapo juu simu hiyo inayojikunja inategemewa kuja na kioo cha inch 4.58 ikiwa imekunjwa na Inch 7.3 ikiwa tablet. Mbali ya hapo pia inasemekana kuwa simu hii ndio itakuwa simu ya kwanza ya Samsung kuwa na uwezo wa mtandao wa 5G.
Mbali na hapo bado tetesi mbalimbali zinaendelea kusambaa mtandaoni, endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuletea tetesi zote kuhusu simu hii mpya ya Samsung inayojikunja.