Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Galaxy S9 Kuja na Aina Mpya ya Ulinzi wa Intelligent Scan

Sasa ulinzi kuongeza ulinzi kwa kuchanganya iris scanner na face recognition
Intelligent Scan kwenye Samsung Galaxy S9 Intelligent Scan kwenye Samsung Galaxy S9

Baada ya kampuni ya Samsung kutangaza rasmi tarehe ya kutoka kwa simu yake mpya ya Samsung Galaxy S9, sasa wataalamu mbalimbali wa mambo ya teknolojia wameanza kuvujisha baadhi ya sifa na muonekano wa simu hiyo kabla ya tarehe halisi ya kutoka kwa simu hiyo.

Hivi karibuni wataalamu kutoka kampuni moja ya huko nchini Korea ya Kusini wamegundua sehemu mpya ya ulinzi ambayo itakuja kwenye Samsung Galaxy S9. Sehemu hiyo ambayo imeitwa “Intelligent Scan” inatarajiwa kuchanganya matumizi ya iris scanner pamoja na face recognition vyote vikifanya kazi kwa wakati mmoja ili kufanya kazi vizuri wakati wa usiku na hata kwenye mwanga hafifu.

Advertisement

Kufafanua hapa inamaana kuwa, wakati unataka kufungua simu yako unatazama simu yako na sensor maalum za iris scanner zita angalia macho yako wakati sensor za face recognition zita angalia uso wako yaani vyote vitafanya kazi kwa pamoja wakati wa mchana au usiku pale itakapo itajika.

Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi juu ya sehemu hiyo, lakini kwa sababu zimebaki siku chache mpaka kutoka kwa simu hiyo mpya. Basi tunategemea kupata ripoti zaidi za sehemu hii hivi karibuni.

Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya Teknolojia, Pakua sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kujifunza mambo yote ya Teknolojia kwa njia ya video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use