Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11)

Simu hizi zinategemewa kuja na muonekano mpya tofauti na simu zilizopita
Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11) Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11)

Kampuni ya Samsung ina jiandaa na uzinduzi wa simu zake za daraja la juu za Samsung Galaxy S20, pamoja na toleo la pili la simu ya kujikunja ya Galaxy Fold 2. Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, Samsung inatarajia kuja na matoleo matatu tofauti ya Galaxy S20 tofauti na kipindi cha nyuma.

Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11)

Advertisement

Samsung inatarajia kuja na Samsung Galaxy S20, Galaxy S20 Plus, pamoja na Galaxy S20 Ultra. Toleo la Galaxy S20 Ultra ndio linasemekana kuwa toleo bora kuliko simu nyingine kwenye matoleo haya ya Galaxy S20.

Japokuwa kwa sasa tetesi ni nyingi sana, lakini naona kikubwa unachotakiwa kujua zaidi ni muonekano mpya wa kamera za simu hizo, ambao sasa unakuja na muonekano wa box liliozinguka kamera zote za nyuma, kama zilivyo simu za Galaxy S10 Lite, na Galaxy Note 10 Lite ambazo zimezinduliwa hivi karibuni.

Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11)

Mbali na hayo simu hizi zinasemekana kuja na kioo cha kisasa cha QHD AMOLED display ambacho kinakuja na uwezo mkubwa wa refresh rate ya hadi GHz 120, pia inasemeka S20 itakuja na uhifadhi wa ndani kuanzia GB 128, GB 256, na GB 512 huku ikisaidiwa na RAM ya hadi GB 12. Vilevile battery za simu hizi zinategemewa kuwa kubwa zaidi kuanzia mAh 4,500 hadi mAh 5,000.

Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11)

kwa upande wa mfumo, Galaxy S20 zinatarajiwa kuja na mfumo wa Android 10.0 huku ikiwa na mfumo wa Samsung One UI 2.0 mfumo ambao umezinduliwa na Samsung hivi karibuni. Mbali na hayo naona tusubiri tu tarehe 11 mwezi wa pili (11 February 2020) mwaka huu ambapo kampuni ya Samsung ndio itaenda kuzindua simu hizi moja kwa moja kupitia mkutano wake utakao fanyika nchini Marekani.

Kwa upande wa Galaxy Fold 2, simu hii inasemekana kuja na processor ya Snapdragon 855 pamoja na RAM ya GB 12 ikiwa pamoja na ukubwa wa ndani kati ya GB 256 hadi GB 512. Simu hii pia inatarajiwa kuja na muonekano mpya ambao sasa simu hii inajikuja kuanzia juu kuja chini tofauti na Galaxy Fold ambayo yenyewe inajikunja kushoto au kulia.

Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11) Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11) Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11)

Kama unavyoweza kuona hapo juu hizo ndio picha za Samsung Galaxy Fold 2 ambayo inatarajiwa kuzinduliwa siku ya tarehe 11 mwezi huo wa pili mwaka 2020.

Kama unataka kuapata taarifa zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku bila kusahau mitandao yetu ya kujamii kwani tutaendelea kukupata taarifa zaidi kuelekea kwenye uzinduzi wa simu hizo mpya kutoka Samsung.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use