Kampuni ya Samsung inategemea kuanza mwaka 2020 kwa simu mpya za Samsung Galaxy S10 Lite na Note 10 Lite. Simu hizi zinakuja kama matoleo mpya ya simu za mwaka 2019 za Samsung Galaxy S10 na Galaxy Note 10.
TABLE OF CONTENTS
Samsung Galaxy S10 Lite
Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, Galaxy S10 Lite inasemekana kuja ikiwa na processor mpya ya Snapdragon 855 SoC, RAM ya GB 8, na uhifadhi wa ndani wa GB 128. Vilevile simu hiyo inasemekana kuja na kioo cha inch 6.7 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya FHD+ Super AMOLED display, huku kioo hicho kikiwa na sehemu ya ulinzi ya fingerprint kwa chini.
Mbali na hayo, Galaxy S10 Lite inasemekana kuja na kamera ya mbele yenye uwezo wa Megapixel 32, pamoja na kamera nyingine tatu za nyuma ambazo zina semekana kuja na uwezo wa Megapixel 48 kwa kamera kuu, Megapixel 12 na Megapixel 5. Kamera zote zinasemekana kuchukua video za hadi 4K.
Hata hivyo kingine ambacho ni cha kufurahia kwenye simu hii ni uwezo wake wa battery, ambapo inasemekana simu hii itakuja na uwezo wa 4,500 mAh battery huku ikiwa na uwezo wa fast charging yenye uwezo wa hadi 45W.
Samsung Galaxy Note 10 Lite
Kwa upande wa Galaxy Note 10 Lite yenyewe inasemekana kuzinduliwa siku yoyote kuanzia leo, huku ikiwa inasemekana kuja na kioo cha inch 6.7 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya FHD na AMOLED. Vilevile simu hii inasemekana kuja na processor ya Exynos 9810 SoC, huku ikiwa inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani wa GB 128.
Kama unavyoweza kuona kwenye picha halisi za simu hiyo zilizovuja hivi karibuni, Galaxy Note 10 Lite inakuja na kamera tatu kwa nyuma ambazo zote zinakuja na ukubwa unaofanana wa Megapixel 12 kila moja lakini kamera zote zinatofautiana uwezo. Kuna kamera ya 12MP telephoto na 12MP ambayo ni ultrawide. Kamera zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video hadi za 4K.
Kwa mbele simu hii inasemekana kuja na kamera ya Megapixel 32 ambayo yenyewe inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps. Galaxy Note 10 Lite inasemekana kuzinduliwa siku yoyote kuanzia leo, huku ikisemekana kupatikana kwa bei ya 630 EUR takribani shilingi za kitanzania TZS 1,617,000 bila kodi.