Hivi karibuni kumekua na uvumi mbalimbali ya kua Samsung nayo huwenda ikachana na pini ya earphone yani (earphone jack). Hatua hizi zimekuja siku chache baada ya kampuni ya Apple kuchukua hatu ya kuachana na (earphone jack) kupitia simu yake mpya ya iPhone 7.
Habari hizo zinaendelea kusema kua samsung imepanga kutengeneza earphone za aina yake ambazo zitakua haziingiliani na zile za iphone 7, hii ikiwa na mana kuwa Samsung imepanga kutengeneza sehemu hiyo tofauti kabisa na iphone na bila kutumia teknolojia ya muundo USB C ambayo ndio inayotumia na iphone 7. Pia habari hizo kutoka kwenye tovuti ya Digital Music News zinaongeza kuwa samsung imepnaga kutengeneza pia earphone zake ambazo zitakua haziingilini kabisa na zile za iPhone na pia tovuti hiyo inabainisha kuwa huwenda Samsung ikatengeneza wireless earphone zake ambazo pia hazito ingiliana na iPhone kwa namna yoyote ile ililisitiza tovuti hiyo.
Katika kujua sababu ya kampuni hiyo kuchukua hatua ya kufanya hivyo, habari zinasema huwenda Samsung wamepanga kutengeneza earphone zenye kutoa sauti zenye ubora zaidi (quality) hii ikiwa ni pamoja na kuamua kuingia kwenye teknolojia mpya kwani pini hizo za earphone (earphone jack) zimesha pitwa na wakati. Hata hivyo kwa mojibu wa tovuti hiyo ya Digital Music News Samsung ili kataa kabisa kuongelea hilo.
Huenda tukawa ndio tunasogelea mwisho wa pini hiyo ya earphone maarufu kama (earphone jack), kwani kama kampuni hizi mbili kubwa (iPhone na Samsung) zote zikiamua kuachana na pini hiyo basi lazima na kampuni zingine zitafuata, ili kupata habari zaidi endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.