Kupitia mkutano wa CES 2020, Kampuni ya Samsung imetangaza bidhaa zake mbalimbali na kupitia makala hii hebu tuongelee kuhusu “Ballie”. Ballie ni roboti mpya kutoka Samsung ambayo imetengenezwa maalum kwaajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za nyumbani.
Kupitia mkutano huo uliofanyika huko Las Vegas nchini Marekani, Samsung imetangaza roboti hiyo ambayo inatumia mfumo wa AI kuweza kuunganisha vifaa mbalimbali ndani ya nyumba yako (smart devices) na kuweza kufanya kazi mbalimbali pale inapo hitajika.
Kwa upande wa upatikanaji, Samsung haikutangaza habari yoyote kuhusu wakati gani roboti hiyo ya Ballie itapatikana kwa wateja duniani, au itauzwa kwa kiasi gani. Kwa hivyo ni ngumu kujua kama haya ni maoni tu ya samsung kwenye siku zinazokuja au kama roboti hii ya “Ballie” itafanikiwa kutoka nje ya mkutano wa CES 2020 na kuwafikia watumiaji duniani kote.
Lakini kwa hivi sasa, endelea kuungana nasi tutakuletea habari zote zilizo jiri kwenye mkutano wa CES 2020, hakikisha unatembelea ukurasa wetu maalum kwaajili ya kupata habari zote zilizojiri kwenye mkutano huo.