Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Video : Sakata la TTCL Kuimiliki Kampuni ya Simu ya Airtel

Hili hapa ndio sakata zima la umiliki wa kampuni ya Airtel kwa TTCL
TTCL Tanzania TTCL Tanzania

Hivi karibuni limeibuka sakata la umiliki baina ya kampuni ya simu ya Airtel pamoja na kampuni ya simu ya TTCL, sakata hilo ambalo kwasasa limechukua sura mpya baada ya mwenyekiti wa bodi ya TTCL kutoa tamko la kuwa wangependa kampuni ya Airtel irudishwa kwa TTCL.

Wakati TTCL ikisema mchakato wa kuirudisha Airtel mikononi mwake utakuwa ni vita kubwa, kampuni ya Bharti Airtel ambayo ndio inayomiliki hisa nyingi za kampuni hiyo ya simu za mkononi, imejitokeza na kusema, Uwekezaji wao ulifuata na kuzingatia sheria na taratibu kabla haujapata baraka zote za Serikali ya Tanzania.

Advertisement

Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi hapo jana, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Omary Nundu akiwa ameambatana na menejimenti ya shirika hilo alizungumza na vyombo vya habari na kusema: “Tunaenda vitani na tunajua hii ni vita kubwa.”

Hata hivyo sakata hili linakuja baada ya siku tatu toka, Rais John Magufuli alipo muagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kufuatilia utata uliopo kwenye umiliki wa kampuni ya Airtel akisema kampuni hiyo ni mali ya Serikali.

Msimamo wa shirika hilo la mawasiliano la Tanzania TTCL kwa mujibu wa Nundu ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano katika Serikali ya Awamu ya Nne ni kwamba hivi sasa hawahitaji tena mgao, bali wanataka Airtel irudishwe katika kampuni ya Serikali. Unaweza kutembelea ukurasa wa mwananchi ili kujua zaidi kuhusu sakata hili.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use