Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Kutoa Simu Mpya ya Galaxy S 8 kwa Wahanga wa Note 7

Kuna tetesi kuwa samsung imepanga kuruhusu wateja wake waliorudisha simu za Note 7 kupata simu mpya ya S 8 kwa bei rahisi
Galaxy S 8 Galaxy S 8

Hivi karibuni kuna tetesi zimesambaa kuwa kampuni ya Samsung inategemea kuwafidia zaidi wateja wake wa Note 7 kwa kuwa raisishia bei ya simu mpya ya Galaxy S 8 ambayo inategemewa kutoka mwezi March mwakani. Taarifa kutoka tovuti mbalimbali zinasema kuwa samsung itafanya hivyo kwa wateja pekee ambao walibadilisha simu zao za Note 7 na kuendelea kutumia simu kutoka katika kampuni hiyo ya Samsung.

Mmoja wa wasemaji wa tovuti moja ya habari za teknolojia aliandika kuwa wateja hao watakadiriwa kiasi cha punguzo kutokana na kama mteja alibadilisha simu yake na kuchukua simu ya Galaxy S 7 na sio simu nyingine. Pia msemaji huyo aliongeza kuwa kampuni ya Samsung bado iko kwenye wakati mgumu kwa sasa kwani inasemekana kutegemea kupunguza baadhi ya viongozi wake wa juu zaidi ya 200 kati ya viongozi 1000 ambao wako kwenye kampuni hiyo.

Advertisement

Samsung ilipata maafa mwezi August mwaka huu baada ya simu zake za Galaxy Note 7 kuanza kulipuka siku chache baada ya kampuni hiyo kuanza kusambaza simu hizo, hata hivyo baadae Samsung iliamua kutangaza kusitisha kabisa usambazaji na uzalishaji wa simu hizo za Note 7 kitendo ambacho kilisababisha kampuni hiyo kupata hasara ya zaidi ya dollar za marekani $17 bilioni ambazo zingepatikana kwenye mauzo na dollar $5 bilioni baada ya kufanya zoezi zima la kurudisha simu hizo.

Inasemekana baadhi ya viongozi wa juu wa Kampuni hiyo bado wanafanyiwa upelelezi kwa kuchangia uzembe uliopelekea hasara kwa kampuni hiyo japo kuwa wa simu hizo zilisha rudishwa tena na kusemekana zilikuwa salama. Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni ya samsung kuamua kupunguza wafanya kazi wake kwani hapo mwaka jana Samsung ili punguza viongozi wake wa juu 129 hiyo huenda labda Samsung wanafanya huu ni utaratibu wa kila mwaka au labda ni kwasababu ya uzembe uliofanyika kwenye Galaxy Note 7 who know’s..?

Je wewe unaonaje Samsung  wamefilisika au ndio namna ya kujipanga..? tuandikie kwenye maoni hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use