Ni Marufuku Kutengeneza Roboti Kwaajili ya Vita au Silaha

Wataalam Wameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua Kuzuia hilo
Roboti Roboti

Wataalamu takribani 100 wa teknolojia ya roboti wameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ili kuzuia kuundwa kwa roboti zinazoweza kuua. Kwenye barua kwa Umoja wa Mataifa, wataalamu wa masuala ya teknolojia akiwemo tajiri Elon Musk, wameonya kuwa hatua hiyo itasababisha kuwepo kwa vita vitakavyo husisha roboti, imeripoti BBC Swahili.

Wataalamu hao wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha. “Wakati zitaundwa, zitawezesha vita kupiganwa kwa kiwango kingine cha juu na kwa haraka zaidi kuliko vile binadamu hufanya.” barua hiyo ilisema.

Advertisement

“Hizi zitakuwa silaha za ugaidi, silaha ambazo magaidi watatumia dhidi wa watu wasio na hatia, na silaha ambazo zitadukuliwa kuhudumu kwa njia ambayo sio nzuri.” iliongeza. Mwaka 2015 zaidi ya wataalamu 1,000 na watafiti waliandika barua wakionya kuhusua kuundwa kwa silaha kama hizo.

Kati ya wale walioweka sahihi barua ya mwaka 2015 ni mwanasayansi Stephen Hawking, na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple Steve Wozniak na bwana Musk. Hata hivyo je roboti za kuua ni zipi?

Roboti za kuua ni silaha ambazo zinaweza kuchagua na kuvamia kitu ambacho zinakilenga bila ya kuelekezwa na binadamu. Tayari kwa sasa zipo lakini kuboreshwa zaidi kwa teknolojia itachangia kuziwezesha kufanya hivyo.

Wale wanao pendelea roboti hizo wanaamini kuwa sheria za sasa za vita zinatosha kutatua shida yoyote ambayo itaibuka ikiwa zitatumiwa. Lakini wale wanaozipinga wanasema kwa roboti hizo ni tishio kwa binadamu na teknolojia yoyote ya kuziwezesha kuuwa inastahili kupigwa marufuku.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : BBC Swahili

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use