Ripoti : Samsung Yaongoza Kwenye List ya Simu Zinazo Nakiliwa Zaidi

Kampuni ya samsung imeongoza kwa kuwa na simu feki ikifatiwa na Apple
Ripoti : Samsung Yaongoza Kwenye List ya Simu Zinazo Nakiliwa Zaidi Ripoti : Samsung Yaongoza Kwenye List ya Simu Zinazo Nakiliwa Zaidi

Kunakili au ku-copy simu ni moja ya kati ya vitu ambavyo vimezoeleka sana hasa kwa siku hizi. Kudhibitisha hilo hivi karibuni, ripoti kutoka kwa watafiti wakubwa wa masoko ya simu za mkononi AnTuTu imetangaza kuwa, Samsung ndio brand ya kwanza inayoongoza kwa kunakiliwa kuliko brand nyingine.

Ripoti hiyo inadai kuwa kati ya makadirio ya nakala za simu janja 17,424,726 zilizo uzwa kwa mwaka 2017, asilimia 2.64% ya simu hizo zilikuwa zimenakiliwa au ni simu feki. Kampuni hiyo pia imetoa chati ya simu zilizoongoza kwa kunakiliwa na Samsung imeshika namba moja kwa kuongoza kwa zaidi ya asilimia 36.23% ya simu zote zilizo nakiliwa, huku simu zake za Samsung S7 zikiwa zinaongoza kwa kunakiliwa.

Advertisement

Hata hivyo Apple nayo ilishika nafasi ya pili kwenye list hiyo kwa mwaka jana 2017 kwa kuwa na simu nyingi zilizo nakiliwa kwa kuchukua asilimia 7.72% ya simu zote zilizo nakiliwa, huku simu ya iPhone 7 Plus ikiwa inaongoza kwa kunakiliwa zaidi. Simu nyingine zilizoongoza kwa kunakiliwa zaidi ni kama inavyo onyesha kwenye chati hapo chini.

Na hiyo ndio ripoti ya simu zilizo ongoza kwa kunakiliwa au kwa kuwa na simu feki zaidi na kama unavyoona kwenye list hapo juu Samsung imeshika kinara, hivyo ni vyema kuwa makini unapo nunua simu za samsung hasa simu za Samsung Galaxy S7.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use