Hivi karibuni ripoti mpya kutoka kwa wataalam wa teknolojia maarufu kama Consumer Reports imedai kuwa simu mpya kutoka kampuni ya Apple, yaani iPhone X ndio simu inayo ongoza kwenye list ya simu zenye kamera bora mpaka sasa.
List hiyo iliyotoleowa na gazeti hilo maarufu, inasema simu ya iPhone X ndio ya kwanza ikifuatiwa na simu nyingine kutoka kampuni hiyo yaani simu ya iPhone 8 Plus, ikifuatiwa na iPhone 8. Bado haijajulikana ni vigezo gani vimetumiwa kuangalia ubora wa kamera za simu hizo huku baadhi ya watu wakiwa wanapingana na list hiyo kwa kile kinacho onekana kutokwepo kwa simu nyingine zenye kamera bora kuliko zile zilizo pangwa kwenye list hii. List nzima iliyotolewa na gazeti hilo ni kama ifuatavyo –
- Apple iPhone X
- Apple iPhone 8
- Apple iPhone 8 Plus
- Samsung Galaxy S8+
- Apple iPhone 7
- Apple iPhone 6S Plus
- Samsung Galaxy S8
- Samsung Galaxy Note8
- Apple iPhone 7 Plus
- Samsung Galaxy S8 Active
List hii ilitolewa rasmi siku ya tarehe 26 mwezi wa pili mwaka huu 2018, wakati baadhi ya simu kama Samsung Galaxy S9 ikiwa ndio imezinduliwa pengine ndio sababu ya simu hii kutokwepo kwenye list hii. Je vipi wewe unaonaje unadhani kweli list hii inafaa kuwa list ya simu 10 zenye kamera bora.? tuambie kwenye maoni hapo chini.