App maarufu ya kutambua muziki ya Shazam hivi karibuni inategemewa kununuliwa na kampuni ya Apple, ripoti zinasema Apple inaweza kutangaza ununuzi huo mapema mwezi huu.
Kwa wale ambao hamjui App ya Shazam, hii ni programu ambayo inakusaidia kutambua jina la muziki pamoja na mashairi ya nyimbo flani. Unachofanya ni kudownload App hiyo kwenye simu yako kisha pale muziki unapoimba basi unabofya kitufe huku unaelekezea mic ya simu yako mahali muziki unapotokea na App hiyo itatambua jina la msanii pamoja na mashairi kama yapo.
Bado haijajulikana Apple wanatanunua App hiyo kwa bei ghani lakini kwa mujibu wa tovuti ya Tech Crush, Apple na Shazam zimepanga kuweka wazi ununuzi wa App hiyo siku ya Jumatatu au jumanne.
Kwa sasa tayari shazam inafanya kazi kwenye mfumo wa SIRI wa simu za Apple ambao sehemu hiyo iliwekwa rasmi kwenye simu hizo miaka kadhaa iliyopita. SIRI inatumia mfumo kuweza kutambua aina ya muziki pale unapo uliza ni aina gani ya nyimbo inaimba kwenye simu yako.
Kama bado huna programu ya Shazam kwenye simu yako unaweza kujaribu programu hiyo kwa kudownload kupitia link hapo chini.
Shazam – iOS
Shazam – Android
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.