Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Remix OS Programu Inayo Badili Simu ya Android Kuwa Kompyuta

Kutana na Remix OS ya simu yenye uwezo wa kubadili simu kuwa kompyuta
Remix OS Remix OS

Ukweli ni kwamba siku hizi watu wengi hutumia simu zenye nguvu pengine kuliko hata baadhi ya kompyuta hasa za zamani, kutokana na sababu hiyo pengine ulishawahi kuwaza kutumia simu yako kama kompyuta au PC. Sasa mwaka huu 2017 hii sio ndoto tena kwani sasa utaweza kutumia simu yako ya Android kama kompyuta kwa asilimia 100.

Kuwezesha hilo kampuni ya Jide Technology imefanikiwa kutengeneza programu ya Remix OS for Mobile programu ambayo itakuwezesha kutumia simu yako kama kompyuta kwa kuichomeka tu kwenye kioo cha kompyuta yako. Akizungumza na mhariri wa tovuti ya Theverge kiongozi wa kampuni hiyo alisema kuwa mteja atahitaji install sehemu ya programu hiyo kwenye simu yake pamoja na kuweka programu ya Google Play kisha baaada ya hapo pale mtumiaji atakapo chomeka simu yake kwenye kioo cha kompyuta programu hiyo humpa muonekano bora pamoja na uwezo wa kutumia keyboard pamoja na mouse kwenye kioo hicho.

Advertisement

Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni za teknolojia kubadilisha simu kuwa kompyuta, kwani hata kampuni ya Microsoft nayo iko mbioni kutoa programu nzima ya Windows 10 kwaajili ya simu za mkononi au smartphone. Kwa sasa programu ya Remix OS iko kwenye hatua za mwisho hivyo hivi karibuni jiandae kuitumia kwanye simu yako na ubadilishe smartphone yako kuwa kompyuta.

Tembelea Tanzania Tech kila siku kwani tutakuletea hatua kwa hatua jinsi ya kuiweka programu hiyo kwenye simu yako pamoja na kuitumia kwenye kompyuta yako. Kwa maelezo zaidi ya programu hiyo unaweza kuyakuta kwenye tovuti hii Jide.com ya kampuni hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use