Kuna wakati mtu unakuwa na haraka ya kutumia kompyuta yako kiasi kwamba unasahau kufuta vitu kwenye recycle bin ya kompyuta yako, kupitia njia hii leo nitakuonyesha njia ambayo unaweza kutumia ili vitu vilivyopo kwenye recycle bin vijifute vyenyewe pale unapozima kompyuta yako.
Kabla ya kuanza labda nikueleze ni maana ya Recycle bin, kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta kwa muda mrefu basi lazima unajua sehemu hii, kama wewe ni mgeni wa kutumia kompyuta basi ni vyema ufahamu kuwa sehemu hii ni ile ambayo ukifuta kitu kinahifadhiwa humo kwaajili ya kusubiria kufutwa kabisa au kuondolewa moja kwa moja kwenye kompyuta yako.
Sasa lengo la maujanja ya siku ya leo ni kusaidia kufuta vitu vilivyomo kwenye Recycle bin pale tu unapozima kompyuta yako, njia hii itakusaidia zaidi kama kompyuta yako ina nafasi ndogo kwani hiitasaidia kuondoa baadhi ya mafile ambayo hayana kazi au hayatumiki tena.
Pia kwa kutumia njia hii itakusaidia kama unatumia kompyuta ambayo sio ya kwako, kwani hii itakusaidia kufuta vitu vyote ambayo ulifuta wakati unatumia kompyuta hiyo ambayo pengine uliazima.
Lakini pia kama unatumia Recycle bin kama sehemu ya kuficha vitu basi njia hii haitokuwa muhimu sana kwako kwani itafanya upoteze mafile yako yote. Basi baada ya kusema hayo twende tukangalie njia hizi.
Kwa kuanza ingia kwenye Desktop yako kisha fungua application ya Notepad kisha copy na paste code hizo hapo chini kwenye ukurasa huo wa Notepad. Bofya hapo chini kucopy code hizo.
Baada ya hapo badilisha format ya .txt na kisha weka .bat alafu Save code hizo kwenye kompyuta yako. Baada ya hapo bofya mara mbili code hizo na utaona vitu vilivyopo kwenye Recycle bin vimefutika, kama havija futika basi angalia labda kuna kitu umekose rudia tena kwa kufuata maelezo kwa usahihi zaidi.
Hakikisa file linasomeka kwa mfano kufuta.bat na sio kufuta.txt, baada ya kufanya hatua hizo hapo juu sasa nenda kwenye sehemu ya ku-search kwenye kompyuta yako kisha andika “gpedit.msc” bila alama za funga na fungua semialafu bofya enter kwenye keyboard yako.
Baada ya hapo litafuguka jedwali lenye jina Local group policy editor, kuwa makini na sehemu hii kwani hapa ndipo panapo endesha kompyuta yako nzima. Baada ya kufungua jedwali hili, upande wa kushoto chagua Windows Settings, kisha utaona page nyingine imefunguka tena kwa chini, Tafuta sehemu iliyo andikwa Scripts (Startup/Shutdown), bofya hapo mara mbili kisha chagua Shutdown kwa kubofya mara mbili.
Baada ya hapo ukurasa mwingine utafunguka kisha bofya sehemu ya Add kwenye kibox alafu bofya Browse kisha chagua mahali ulipo hifadhi zile code zenye jina kwa mfano kufuta.bat kisha bofya Open. Baada ya hapo utakuwa umemaliza zoezi zima na sasa utakuwa upo tayari kufuta mafile yako kwenye recycle bin kila mara unapozima kompyuta yako.
Hiyo ndio njia rahisi unayoweza kutumia pale unapotaka kufuta mafile kwenye recycle bin kwa haraka, kama unataka kujua njia nyingine ya kufanya kompyuta yako ifanya kazi haraka kwenye internet unaweza kusoma hatua kwa hatua hapa. Kwa maujanja zaidi kama haya hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.
Kama kuna mahali umekwama au hujaelewa unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tutakujibu kwa haraka.
Muundo wa website yenu nimeupenda sanaaa