Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Re-Volt3 Game Mpya ya Magari Kwaajili ya Mfumo wa Android

Kama wewe ni mpenzi wa game za kwenye mifumo ya android basi game hii mpya ya magari ya Re-Volt3 ni kwaajili yako
re-volt3 re-volt3
taaaaaa

Kampuni maarufu ya teknolojia ya WeGo Interactive hivi karibuni imetangaza ujio wa game yake mpya ya Re-Volt3 kwenye mfumo wa Android. Game hiyo mpya ambayo imetengenezwa maalumu kwa wapenda mbio za magari ni moja kati ya game bora na za kisasa zenye muonekano (graphics) halisi kutoka kampuni hiyo yenye mako yake makuu huko Guro-gu Seoul nchini Korea.

Game hiyo mpya inajumisha zaidi ya magari 50 yakiwemo magari makubwa, wachezaji wa game hiyo wanauwezo wa kubadilisha rangi ya magari hayo pamoja na vitu vingine ili kuweka  jinsi wanavyotaka. Vilevile game hiyo inashirikisha wachezaji wawili pale mtu anapotaka kucheza online ili kushindana na mwenzake, hata hivyo game hiyo inazo level zaidi ya 100 ambazo zitamfanya mchezaji kupanda daraja kila atakapo maliza level moja kwenda nyingine.

Advertisement

Kama unataka kujaribu game hiyo kwa sasa inapatikana Play Store hivyo unaweza kuipakua game hiyo moja kwa moja kutoka huko au bofya hapo chini kama unatumia mfumo wa Android.

Kama umesha pakua game hiyo tuandikie maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use