Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet

Utaweza kutumia ramani live bila kutumia Internet kwenye simu yako
Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet

Kama wewe ni mtumiaji wa smartphone ya aina yoyote basi ni wazi kuwa ramani au maps ni moja kati ya kitu kina chofanya simu yako kuwa smart. Kupitia ramani unaweza kwenda sehemu yoyote ile kwa kufuata maelekezo ya ramani kupitia simu yako hata kama ujawahi kufika sehemu husika.

Mbali ya hayo pia utaweza kufanya mambo mbalimbali kama kujua umbali kati ya sehemu na sehemu na mambo mengine kama hayo. Mbali na kuweza kufanya mambo yote hayo tatizo la sehemu ni lazima kutumia Internet kwenye simu yako au kuwasha data ndipo uweze kutumia ramani kwenye simu yako.

Advertisement

Kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi ya kutumia ramani kwenye simu yako bila kutumia data au bila kuwasha data kila wakati unapotaka kupata location ya eneo.

Basi bila kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye hatua hizi, kitu cha muhimu hakikisha unafuata maelekezo yote kwenye makala hii. Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini, kisha baada ya hapo fungua app hiyo na fuata maelekezo yafuatayo.

Njia ya Kwanza

Kama unataka kutumia ramani kupitia app ya Google Map bila kutumia Internet basi njia hii ni bora kwako. Unacho takiwa kufanya ni kufungua app ya Google Map, kisha moja kwa moja boya sehemu ya kutafuta au Search ambayo ipo juu kabisa kwenye app ya Google Map.

Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet

Kupitia sehemu hiyo andika maneno “Ok Map” moja kwa moja utaweza kuona Google ikitengeneza ramani rasmi ambayo unaweza kutumia bila internet.

Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet

Baada ya hapo bofya kitufe cha Download na kisha moja kwa moja utaweza kutumia seheu hiyo ya ramani kupitia simu yako bila kutumia Internet kabisa. Kitu cha muhimu hakikisha wakati unafanya hatua hizi za awali ni vizuri kuwa na Internet ili kupakua sehemu ya ramani ambayo utaitumia baadae bila kuwa na Internet au Data.

Njia ya Pili

Njia hii ya pili ni rahisi zaidi kama umeona njia ya kwanza ni ngumu kwako, unachotakiwa kufanya ni kupakua app kupitia link hapo chini, kisha endelea kwa kufuata maelezo zaidi hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload fungua app hiyo moja kwa moja bofya sehemu ya Get Started iliyopo chini kabisa kwenye app hiyo.

Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet

Baada ya hapo, moja kwa moja kwenye ukurasa unafuata subiri kidogo kisha moja kwa moja utaletewa ramani unayotakiwa kuhifadhi kwenye simu yako. Bofya kitufe cha Download na moja kwa moja subiria sehemu ya ramani hiyo iweze kuhifadhiwa kwenye simu yako.

Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet

Baada ya hapo utaletewa ujumbe ambao unakuhitaji kuunganisha app hii na data na utaweza kutumia MB 72 tu kuweza kupakua ramani hii kama upo hapa Dar es salaam. Kama upo mikoani unaweza kupakua kwa MB chache zaidi kulingana na ukubwa wa ramani.

Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet

Baada ya kupakua ramani na kuhifadhi kwenye simu yako moja kwa moja bofya sehemu ya Show iliyopo chini kwenye sehemu ilipokuwa ina download ramani husika.

Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet

Baada ya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa ramani ambapo sasa unaweza kutafuta eneo lolote na kupata location yake bila kutumia data. Ili kuhakikisha unapata umbali kutoka eneo ulilopo washa GPS kwenye simu yako bila kuwasaha data kisha bofya sehemu ya target kuweza kupata eneo ulilopo.

Jinsi ya Kutumia Ramani (Map) Kwenye Simu Bila Internet

Unaweza kutumia app hii kuona njia za kwenda kutoka eneo moja hadi lingine bila Internet, na utaweza kutumia live location pia bila Internet. Kitu cha msingi hakikisha unawasha GPS kwenye simu yako ili kupata location halisi.

Kwa kutumia njia hii natumaini kuwa utakuwa umeweza kutumia ramani kwenye simu yako kwa urahisi bila kutuia Internet. Kama unataka kujua maujanja zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kupata network sehemu ambapo hakuna network kwa kutumia ramani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use