Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

ProtectPax Screen Protector ya Kupaka Ngumu Kuliko Zote

Screen protector iliyoko kwenye mfumo wa kimimina
Screen Protector Screen Protector

Ni mara nyingi sana una kwaruza, unavunja au pengine unaharibu kioo cha simu yako bila hata kutegemea. Yote hayo yanakomeshwa na screen protector iliyoko kwenye mfumo wa kimiminika ya ProctectPax, hii ni aina mpya ya screen protector ambayo ni ngumu kuliko zote duniani na ni bora kuliko screen protector zote ninazo zijua kwa sasa.

ProtectPax imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya Nanotechnology ambayo inasaidia kioo cha simu yako kuwa na ulinzi wa asilimia 100, haijalishi simu yako imeanguka, umemwagia maji au hata umekwaruza kioo cha simu yako screen ptotector hiyo itaendelea kulinda kioo cha simu yako kwa ubora uleule. Zaidi ni kuwa ubora wa screen protector hiyo huishii kwenye kulinda simu yako bali hata muonekano wake kwani hii huwa sambamba kabisa na simu yako hivyo ukiweka kwenye simu yako haionekani kabisa kwa asilimia 99.

Advertisement

https://www.instagram.com/tv/CA7s3ZIAt5k/?utm_source=ig_web_copy_link

Kuweka screen protector hii hauitaji utaalamu wa aina yoyote bali utakachofanya ni kufuta kioo chako kisha utamimina kimiminika hicho kwenye kioo cha simu yako na kusambamba kwa kidole kisha baada ya dakika 10 screen protector hiyo itakauka na kuwa sambamba na kioo cha simu yako huku kikiwa safi kabisa bila kuacha nafasi wala upenyo wowote. ProctectPax inauwezo wa kulinda kitu chochote kunzia kompyuta, simu, saa ya mkononi, miwani au kitu chochote chenye kioo kwa mbele. Protector hiyo inategemewa kuingia sokoni kuanzia mwezi april na bado haijajulikana bei halisi ya protector hizo.

Kupata habari zaidi unaweza kujiunga na App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi pia ungana nasi kupitia Tanzania Tech Channel ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use