Kompyuta ni kifaa muhimu sana kwa kazi za kila siku, hii ni wazi kwa wafanyakazi wa ofisini pia pamoja na wanafunzi wa level mbalimbali.
Katika kuanza mwaka mpya 2022, ni wazi mambo mengi huanza mwanzo hii ikiwa pamoja na mfumo mzima wa kufanya kazi. Kuliona hilo hivi leo nimekuletea list ya programu za muhimu kutumia kwenye kompyuta yako, programu ambazo naamini zitaweza kusaidia sana kufanya mambo kwa haraka na urahisi zaidi.
Programu hizi ni maalum kwa watumiaji wa mfumo wa Windows, na unaweza kutumia kwenye mifumo yote ya Windows yaani Windows 7, Windows 10 pamoja na mfumo mpya wa Windows 11.
Basi baada ya kusema hayo bila kupoteza muda, moja kwa moja twende kwenye programu hizi za muhimu kuwa nazo kwenye kompyuta yako.
TABLE OF CONTENTS
Clip
Clip ni programu ambayo itakusaidia kutuma mafail au link kwa haraka kutoka kwenye kompyuta yako kwenda kwenye simu yako. Programu hii inaweza kukupa uwezo pale unapo nakili kitu kwenye kompyuta yako unaweza kukiweka moja kwa moja kwenye simu yako bila kutumia waya.
Unaweza kufahamu zaidi kuhusu programu ya clip kwa kusoma hapa. Programu hii inafanya kazi kwenye simu zote za Android pamoja na iOS, pia unaweza kutumia kwenye kompyuta za Windows pamoja na Mac.
File Converter
Unaweza kuthani kua huitaji programu ya kubadilisha format za mafile kwa urahisi (File Converter), lakini ukweli ni kwamba unahitaji programu hii sana. Programu hii ya File Converter ni tofauti kabisa na programu nyingine kwani hii itakusaidia kubailisha mafile ya aina zote kwa haraka na urahisi.
Utaweza kubadilisha format za mafile kwa kubofya tu kitufe cha kulia kwenye mause yako kisha changua format unayota na moja kwa moja utaweza kubadilisha format ya file husika. Unaweza kusoma zaidi kuhusu programu hii hapa.
Everything
Kama wewe ni kama mimi na umekuwa na mafaili mengi kwenye kompyuta yako na ungependa kutafuta mafaili kwa haraka basi programu ya everything ni bora zaidi kwako.
Programu hii inafanya kazi vizuri sana na haraka kuliko sehemu ya kutafuta ambayo inakuja na mfumo wa Windows. Kizuri zaidi ni kuwa programu hii inakuja na size chini ya MB 5. Unaweza kusoma zaidi kuhusu programu hii hapa.
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hupenda kushare kazi zako kwa kuchukua screenshot basi programu hii ni muhimu kuwa nayo. Najua kuwa inawezekana unajua jinsi ya kuchukua screenshot kwa kutumia mfumo wa Windows bila programu yoyote.
Lakini programu hii ni bora zaidi kwa kuwa inakupa uwezo zaidi ya kuchukua screenshot. Kupitia programu hii utaweza kuchukua screeshot za aina mbalimbali ikiwa pamoja na uwezo wa kushare kwa urahisi na haraka. Trust me! unahitaji programu hii kwenye PC yako.
WhatsApp PC
Ni wazi kuwa programu ya WhasApp ni moja ya promu muhimu sana, lakini hadi hivi karibini ilikuwa ni lazima simu yako iwe na internet ndipo uweze kutumia WhatsApp kwenye kompyuta.
Lakini kwa sasa huna haja ya kuwasha simu yako au simu yako kuwa na Internet ndipo uweze kutumia WhatsApp kwenye kompyuta. Hii inafanya programu ya WhatsApp kuweza kutumia kwenye kompyuta yako bila wewe kushika simu yako kila wakati meseji itakapo ingia.
Hii itasadia kama unatumia WhatsApp kuwasiliana na wafanyakazi wenzio au hata wanafunzi wenzako, hivyo ni muhimu sana kuwa na WhatsApp kwenye kompyuta yako. Unaweza kusoma zaidi hapa kujua jinsi ya kutumia WhatsApp kwenye PC bila simu yako kuwa na Internet.
Cloudflare Wrap
Kama wewe ni mtumiaji wa Internet mara kwa mara na unataka kutumia internet kwa haraka huku data zako zikiwa salama kwenye kompyuta yako, basi ni muhimu kufahamu programu ya Cloudflare Wrap.
Kwa ufupi kabisa programu hii hufanya kazi kama VPN lakini ikiwa inakuja na ubora zaidi kwa kubadilisha DNS za kompyuta yako na hivyo kufanya Internet kuwa haraka zaidi. Mbali ya hayo pia itasaidia kuzuia data zako zisiweze kuchukuliwa na kampuni nyingi za ISP. Kama kazi zako zinatumia Internet zaidi basi programu hii ni muhimu sana kwenye PC yako.
Unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutumia programu hii kwenye simu yako ya Android ili kuongeza kasi ya Internet.
Hitimisho
Na hizo ndio baadhi ya programu za muhimu kuwa nazo kwenye kompyuta yako ambayo inatumia mfumo wa Windows. Kumbuka ni muhimu kufahamu kuwa list hii sio programu za kila siku kwani naamini kwenye kompyuta yako tayari unazo programu ambazo unahitaji.
Programu hizi ni zile ambazo na uhakika baada ya kutumia simu moja utaweza kuendelea kutumia kila siku kutokana na kurahisha kazi zako za kila siku kwenye kompyuta.
Ahsante sana kwa makala hii
Naomba kusaidiwa jinsi ku-factory reset Laptop
Angalia kwenye settings ya simu yako