Jinsi ya Kutumia Programu za Adobe Bure Bila Kulipia (Windows)

Kupitia njia hii utaweza kutumia programu zote za Adobe
Jinsi ya Kutumia Programu za Adobe Bure Bila Kulipia (Windows) Jinsi ya Kutumia Programu za Adobe Bure Bila Kulipia (Windows)

Adobe ni moja kati ya programu za muhimu sana kuwa nazo, programu hizi zimekuwa ni za muhimu kiasi kwamba ni ngumu kwa mtu yoyote anayefanya maswala ya graphics kuendelea kufanya kazi hizo bila kuwa na programu hizo.

Kupitia makala ya leo nitaenda kuonyesha njia ambayo unaweza kutumia ili kuwezesha programu zote za Adobe za mwaka 2019 bure bila kulipa gharama yoyote. Kumbuka makala hii ni kwa ajili ya kujifunza hivyo ni muhimu sana kuzingatia vigezo na masharti ya utumiaji wa programu zote za Adobe.

Advertisement

Kupitia njia hii utaweza kutumia programu zote za Adobe ambazo zinapatikana kwenye list hapo chini.

  • Adobe Photoshop CC 2019
  • Adobe Dreamweaver CC 2019
  • Adobe Premiere Pro CC 2019
  • Adobe After Effects CC 2019
  • Adobe Audition CC 2019
  • Adobe Illustrator CC 2019
  • Na nyingine…

Sasa unachotakiwa kufanya ingia kwenye tovuti ya Adobe kisha tengeneza akaunti na download Adobe Creative Cloud, baada ya hapo install kwenye kompyuta yako kisha fungua programu hiyo alafu download programu ya Adobe unayo hitaji.

Jinsi ya Kutumia Programu za Adobe Bure Bila Kulipia (Windows)

Kama unaona njia hiyo ni ngumu unaweza kutumia njia hii ambayo nahisi ni rahisi. Ingia kwenye tovuti hii kisha shuka mpaka chini kidogo kisha utaona Sehemu ya kudownload kwenye tovuti hiyo ipo chini kabisa na kumbuka hakikisha unachagua mfumo wa Windows kama ilivyo onyeshwa kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kutumia Programu za Adobe Bure Bila Kulipia (Windows)

Baada ya kudownload unaweza kuinstall programu hiyo kisha endelea kwenye hatua inayofuata.

Bofya hapa kuweza kudownload file linaitwa Adobe cc 2019, ndani ya hili file kuna files za kila programu ya Adobe unayotaka kutumia. Unachotakiwa kufanya ni kuzima internet kwenye kompyuta yako kisha Copy File moja la programu husika mfano adobe photoshop lililopo kwenye folder la Adobe cc 2019.

Alafu Right Click kwenye programu ya yoyote ya adobe uliyo install mfano Adobe photoshop kisha bofya open file location alafu paste file hilo kwenye location hiyo.

Jinsi ya Kutumia Programu za Adobe Bure Bila Kulipia (Windows)

Hakikisha file ulilo Copy linafanana na programu unayotaka kutumia pia hakikisha sehemu unayo paste file hilo inafanana na kama picha hapo chini.

Jinsi ya Kutumia Programu za Adobe Bure Bila Kulipia (Windows)

Baada ya hapo utakuwa umemaliza na sasa unaweza kutumia programu ya Adobe bure bila kulipia kitu chochote. Kumbuka kama kuna mahali ujaelewa unaweza kuuliza swali lako hapa, au kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Kwa maujanja zaidi kama haya hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku, pia kama unataka kujifunza kwa vitendo maujanja mbalimbali hakikisha una subscribe kwenye channel yetu hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use