Kuna wakati unajikuta na mambo mengi kiasi kwamba huwezi kuangalia TV nyumbani kwako hii inakufanya ugeukie kwenye kitu kimoja ambacho uko nacho kila saa ambacho ni simu yako ya mkononi. Zifuatazo ni programu ambazo zitakuwezesha kuangalia kwa urahisi TV kwenye simu yako ya Mkononi yenye mfumo wa Android.
- Simu TV
Simu TV ni programu ambayo itakuwezesha kuangalia TV na mara nyingi programu hii ni nzuri kama wewe unapendelea kuangalia taarifa ya habari pamoja na matukio mengine yanayotokea hapa Tanzania.
- ITV Tanzania
ITV Tanzania ni programu ambayo inakusaidia kuangalia channel ya ITV pamoja na vipindi vyote vinaoonyeshwa kwenye channel hiyo ya hapa Tanzania.
- VidTV
VidTV ni programu inayokuwezesha kuangalia TV mbalimbali hasa TV za Afrika Mashariki, programu hii inayo channel mbalimbali za habari, michezo na burudani.
- SPB TV – Free Online TV
SPB TV ni programu ya kuangalia TV kwenye simu ambayo inakuwezesha kuangalia channel mbalimbali za nje zaidi ya 200, programu hii inayo watumiaji zaidi ya milioni 40.
- Crackle – Free TV & Movies
Crackle ni programu inayokupa uwezo wa kuangalia Movies na Live TV kwenye simu yako, kwa kutumia programu hii utapata uwezo wa kuangalia filamu na tamthilia mpya na zamani kutoka nje ya nchi.
- NBC
Kwa kutumia programu hii ya NBC utaweza kuangalia Tamthilia mpya mbalimbali moja kwa moja kwa kutumia simu yako.
- FilmOn Free Live TV & RECORD
Programu hii pia ni programu kwaajili ya simu yako inayokuwezesha kuangalia michezo, burudani Tamthilia pamoja na filamu mbalimbali.
- JioTV Live Sports Movies Shows
Jio TV ni programu ambayo inakuwezesha kuangalia michezo, habari, burudani na filamu vyote kupitia simu yako ya mkononi, programu hii ina channel mbalimbali pamoja na channel zaidi ya 20 zenye teknolojia ya HD.
- ESPN
ESPN ni programu inayokuwezesha kuangalia habari mbalimbali za michezo, programu hii inakupa habari za michezo kwa muundo wa makala na pia inakupa habari kwa njia ya TV.
Na hizo ndio baadhi tu ya programu zitakazo kuwezesha kuangalia TV kwenye simu yako, Sasa huna haja ya kukimbia nyumbani kuangalia TV kwani sasa una TV kwenye simu yako ya Mkononi ya Android. Kwa habari zaidi unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store au kama unataka kujifunza teknolojia kwa njia ya Video kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube.
Asante kwa kutungua macho naulizia yenye kuonyesha live matches za u.k, Hispania bila kulipua yani free