Kama unavyojua kutafuta programu bora ya Android ni jambo gumu sana kwani siku hizi kuna programu nyingi sana ambazo zipo kwenye masoko mbalimbali mtandaoni, lakini leo tanzania tech tunakukusanyia programu bora za android ambazo hufanya kazi mbalimbali ili kurahisisha maisha na kufanya smartphone yako kuwa rahisi kutumia.
Kumbuka pia programu hizi zinaendelea kuongezwa kadri tunapoziona programu bora siku hadi siku hivyo ni vye kupitia post hii kila siku ili kuona programu gani imeongezwa katika listi hii.
Ulinzi wa Neno la Siri (Password)
Kuandika password kila mara au kila wakati unapo-takiwa ni kazi sana na kuna wakati kwa namna moja ama nyingine unasahau password hizo ndio maana watengenezaji wa programu ya Dashlane wakafikiria kutengeneza programu hii. Programu hii itakusaidia kuhifadhi password zako ili kama unapotaka kutumia iwe rahisi hata hivyo uhifadi wa password kwa kutumia programu hii ni rahisi sana kwani pale unapotaka kutumia password zako programu hii itakuruhusu kucopy password zako na kuzi paste katika sehemu inayotakiwa. Zaidi ni kwamba programu hii inauwezo wa kuifadhi kadi zako za benki ili pale unapotaka kufanya manunuzi iwe rahisi pia kuhusiana na swala la ulinzi programu hii inatumia ulinzi wa hali ya juu ili kufanya nyaraka zako zote kuwa salama.
Hali ya Hewa (Weather)
Kuna programu nyingi sana za hali ya hewa mbazo zinakuja tayari zimesha hifadhiwa ndani ya simu yako programu hizi zinakua na muonekana mzuri na pia huonyesha hali ya hewa kwa usahihi lakini kama unataka programu yenye uwezo mkubwa na muonekano mzuri programu ya MoreCast ni programu yako, programu hii ina uwezo wa hali ya juu kuanzia kulinganisha hali ya hewa ya miji miwili mpaka kuonyesha hali ya hewa sahihi kwa wakati unaostahili.
Kizinduzi Bora (Launcher)
Vizinduzi au launchers zinafanya muonekano wa simu yako kubadilika kuanzia icon za simu yako, wallpapers na muonekano mzima wa simu yako unaweza ukatafuta launchers hizi mbalimbali kwenye Play Store ili ujionee jinsi zinavyofanya simu yako iwe nzuri, lakini kwa leo tanzania tech tunaku-shauri kutumia launcher ya Action Launcher 3 hii ni launcher bora kwani inakupa muonekano bora wa simu yako na kukufanya ukiona simu yako ni mpya kabisa ijaribu sasa bofya link hapo chini kupakua moja kwa moja kwenye Play store.
Afya na Mazoezi (Health and Fitness)
Iwe unataka kupunguza uzito au unataka tuu kuongeza nguvu na afya bora kwenye mwili wako programu ya 7 Minute Workout ni programu bora ya kutumia kwenye simu yako ya android programu hii inakupa uwezo wa kufanya mazoezi madogo madogo ambayo yatapelekea mwili wako kujengeka vizuri kwa Afya uku ikikuacha ukiwa fit! na mwenye nguvu, ijaribu sasa programu hii pakua kwa kubofya hapo chini.
Ulinzi na Kizuizi cha Virus (Antivirus)
Ulinzi wa simu yako ni kitu cha kuzingatia sana tena ukizingatia simu nyingi za android zinauwezo wa kuingia virus ambazo zinaweza zikafanya simu yako kuwa na hali ambayo haieleweki, hivyo ni vizuri ukaweka anti-virus ili kusaidia ulinzi wa simu yako na kuepuka kwenda kwa fundi kila saa, kama unataka kufanya hivyo tungependa kukushauri kutumia programu ya Mobile Security & Antivirus inayotengenezwa na kampuni maarufu ya avast, programu hii inakupa ulinzi wa hali ya juu na hautajuta kuipakua.
Internet na Kisakuzi (Browser)
Kutumia internet ni kila kitu kwenye smartphone za siku hizi lakini kuna wakati kisakuzi au browser ya simu yako inakufanya uone simu yako haiko vizuri, yote hii ni kwa sababu ya kisakuzi cha simu hakifanyi kazi vizuri inavyotakiwa ndio maana tunakushauri kutumia kizasakuzi cha Google Chrome Beta, kisakuzi hichi kinakupa uwezo wa kutumia sehemu mpya ambazo zinakuja kwenye programu hiyo. Lakini kwa kutumia programu hii kuna wakati unaweza kuona matatizo madogo madogo kwa kua programu hii ni Beta Version. Kumbuka kuwa matatizo haya hayawezi kuadhiri simu yako kabisa hivyo, ijaribu sasa Google chrome Beta ujionee mwenyewe inavyo fanya kazi ipakue hapo chini.
Vipindi na Radio Mtandao (Podcast)
Kama unatafuta vipindi mtandaoni pamoja na radio mtandaoni zipo baadhi ya programu nzuri ambazo zinauwezo wa kufanya hivyo lakini programu ya Podcast Addict ni programu bora ya bure inayokupa vipindi mbalimbali vya mtandaoni na kikubwa zaidi ni ya bure kabisa, hivyo usisite kuipakua programu hii kwani inafanya kazi inavyotakiwa pakua programu hii hapo chini.
Kiandishi cha Maneno (Keyboard)
Kama unatafuta programu bora ya kukusaidia kuandika kwenye simu yako unaweza kupata programu nyingi sana kwenye Play Store lakini kwa leo keyboard bora ya kutumia ni Fleksy programu hii inauwezo mzuri na ina muonekano bora kabisa na inafanya kazi kama inavyotakiwa jaribu sasa kwa kuipakua hapo chini.
Kipakuzi Muziki (Music Downloader)
Kama unataka kupakua muziki bure kabisa na kwa uhalali unaweza kutumia programu hii ya android ambayo imetengenezwa na wale wataalamu wa mtandao Google, programu hii ni bora kabisa na kizuri ni kwamba inakupa uwezo wa kupakua muziki bure na halali kabisa programu hii ni Google Play Music ipakue sasa hapo chini.
Habari na Muhtasari (News and Breaking News)
Kama unataka kupata habari mbalimbali zinazotoka ndani ya tanzania pamoja na taarifa mbalimbali za michezo siasa, burudani na nyingine nyingi ni vyema ukapakua programu ya Millard Ayo programu hii ni bora na inaweza kukufanya kuwa na uhakika wa kupata habari moja kwa moja, pakua programu hiyo hapo chini.
Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.