Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Programu 8 Bora za Antivirus Kwaajili ya Kompyuta Yako

Hizi ndio Programu 8 bora za kutumia kwenye kompyuta yako ili kuzuia Virus
antivirus antivirus

Likija katika swala la ulinzi wa kompyuta yako hakuna kitu cha muhimu kama kuchagua Antivirus yenye uwezo kamili wa kuilinda kompyuta yako kwani kuna aina nyingi sana za antivirus ambazo nyinginezo hazifanyi kazi kama zinavyotakiwa, unaweza kukuta antivirus hii inauwezo wa kuondoa virus wa aina fulani nyingine haina na hii ndio sababu leo tanzania tech tunakuletea machaguo 8 ya programu za antivirus ambazo zitaweza kuweka ulinzi kamili kwenye kompyuta yako.

Kaspersky Total Security

Advertisement

Kaspersky Total Security ni programu ya kisasa ya ulinzi yenye uwezo mkubwa sana wa kulinda kompyuta yako na pia simu yako yenye kutumia Android kwani programu hii inapatikana pia bure kwenye mfumo wa Android.

Sifa za Kaspersky Total Security

  • Ina weka ulinzi kwenye kompyuta na simu yako bila kusababisha simu au kompyuta yako kuwa taratibu (Slow).
  • Ina Uwezo wa kulinda picha zako,mafaili ya muhimu pamoja na data zote za siri.
  • Ina Uwezo wa kulinda nywila (password) zako na kuzihifadhi kwenye usalama kwa aajili ya matumizi ya baadae.
  • Inaweka usalama kwa watoto wako kwa kuzuia watoto kutembelea aina flani za tovuti
  • Ina Uwezo wa kulinda nyaraka zako kwenye kompyuta na kwenye internet
  • Ina Uwezo mkubwa wa kuondoa aina nyingi za virus

Download Kaspersky

McAfee LiveSafe

McAfee LiveSafe ni moja kati ya programu bora za antivirus na ni kati ya programu chache ambapo zimewahi kushinda tuzo ya kuwa programu bora ya antivirus. Programu hii pia inapatikana kwenye mfumo wa android hivyo inakusaidia kulinda simu yako ya android sawasawa na unavyolinda kompyuta yako.

Sifa za McAfee LiveSafe

  • Inauwezo wa kulinda komyuta yako na simu yako pale unapokua mtandaoni
  • Inazuia uwezekano wa mtumiaji kupakua mafaili yenye virus kwenye simu au komyuta yako.
  • Inauwezo wa kuhifadhi nywila (password) zako na kuziweka sehemu salama kwaajili ya matumizi ya baadae.
  • Inauwezo wa kulinda memory yako iliyoko mtandaoni (Cloud Storage)

Download MacFee

Symantec Norton 360

Symantec Norton 360 ni moja kati ya programu zinazojulikana sana programu hii inauwezo wa kulinda mpaka kompyuta 10 kwa leseni moja, pia programu hiyo inauwezo wa kulinda kompyuta yako kutokana na virusi vya Trojans, Malware pamoja na matatizo mbalimbali yanayotokana na mtandao.

Sifa za Symantec Norton 360

  • Ina uwezo wa kulinda kompyuta 10 kwa leseni moja tu.
  • Ina uwezo wa kukulinda pale unapofanya manunuzi kwenye mtandao.
  • Ina uwezo wa kuzia watoto kutembelea baadhi ya tovuti kwenye kompyuta.
  • Ina kupa kiasi cha GB 25 kwaajili ya kuhifadhi data zako kwenye server zenye ulinzi wa hali ya juu.
  • Inakupa taarifa ya programu zenye virus kabla hauzajipakua kwenye kompyuta yako
  • Inapatikana kwenye vifaa vya android hivyo unaweza kutumia leseni hiyohiyo ambayo umenunua.
  • kwa kutumia programu hiyo unauwezo wa kurudishiwa pesa zako pale utakapo ona programu hiyo haikufai.

Download Symantec Norton 360

Avira Internet Security Suite

Avira Internet Security Suite  hii ni programu nyingine  ya anti virus yenye uwezo mkubwa wa kulinda kompyuta yako dhidi ya virus za aina ya Trojans, email zenye virus pamoja na malware za aina zote.

Sifa za Avira Internet Security Suite

  • Avira Internet Security Suite imetengenezwa kwa teknolojia mpya ya kisasa hivyo programu hii inatoa ulinzi mzuri na wa kisasa.
  • Programu hii inayo uwezo mkubwa wa kugundua virus za aina ya Mailware hivyo kama unahisi kompyuta yako inayo malware za aina yoyote programu hii ni bora sana kwako.
  • Ina uwezo wa kulinda kompyuta yako bila ya kusababisha komyuta yako kuwa taratibu (slow).
  • Avira Internet Security Suite inayo programu maalum yenye kusaidia kusafisha ma file ya kompyuta yako ili kuongeza ufanisi zaidi kwenye kompyuta yako.

Download Avira Security

AVG Ultimate

AVG Ultimate ni aina nyingine ya antivirus ambayo inauwezo mkubwa wa kulinda kompyuta yako pamoja na mafile ya kompyuta yako, programu hii ni bora kwa matumizi ya nyumbani kulinda kompyuta za nyumbani na kuongeza ulinzi zaidi kwa kompyuta ya nyumbani.

Sifa za AVG Ultimate

  • Inazuia Virus Malware na virus za aina nyingine
  • Ina Uwezo wa kukupa ulizi dhidi ya Hackers
  • Ina Uwezo wa kuongeza nafasi ya Hard disk yako kwa kuondoa file na programu zisizo tumika.

Download AVG Ultimate

F- Secure

Hii ni aina nyingine ya antivirus ambayo iko siku nyingi sana zaidi ya miaka 25 mpaka sasa programu hii bado inafanya vizuri na ni moja kati ya programu chache ambazo ni bora.

Sifa za F- Secure

  • Ina uwezo mzuri wa kuweka ulinzi kwenye internet
  • ina uwezo mzuri wa kuzuia malware za aina zote pamoja na virus kama vile trojan.
  • Pia inakupa uwezo wa kusafisha kompyuta yako kwa kutumia programu maalumu ya F-secure online scanner.

Download F Secure

ESET NOD32 Antivirus

Programu hii ni moja kati ya programu za kisasa zenye uwezo mkubwa wa kulinda kompyuta yako na vilevile simu yako. Pia programu hii inauwezo wa kuongeza uwezo wa komyuta yako kama unatumia kompyuta yako kwaajili ya kucheza Game.

Sifa za ESET NOD32 Antivirus

  • Programu hii inauwezo wa kuzuia karibia asilimia 80 ya virus zote zinazopatikana kwenye mtandao
  • Programu hii inapatikana kwenye android pamoja na komyuta hivyo inakupa ulizi wa vifaa vyako kwa wakati mmoja.
  • Inayo sehemu maalumu ambayo inaitwa Gamer Mode ambayo inakuwezesha kuongeza ngovu ya kompyuta yako ili kuwezesha kucheza game kwa urahisi zaidi.

Download ESET NOD32

eScan Antivirus

eScanAV Anti-Virus Toolkit (MWAV) ni programu ambayo inakusaidia kuondoa virus kwenye vifaa vako kama vile flash na vitu vingine kama hivyo, na pia inauwezo mkubwa wa kuondoa virus kama vile trojana, win32 pamoja na wengine wengi.

Sifa za eScan Antivirus

  • Ina kusaidia kuondoa virusi kwenye USB Flash
  • Inachukua memory ndogo pengine kuliko anti virus nyingine zozote zile inatumia kiasi cha MB 10 tu kwenye kompyuta yako.
  • Kwa kutumia eScan unaweza kugundua link zenye virus kabla hauzaji zipitia.

Download eScan

Hizo ndio baadhi tu ya programu ambazo ni bora kutumia kwenye kompyuta yako unaweza kupakua programu hizo ili kujaribu moja kwa moja.

Ili kujua zaidi kuhusu ulinzi wa kompyuta yako endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use