Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta wa siku nyingi au hata kama wewe ni mtumiaji mpya wa kompyuta lazima utakua unajiuliza programu zipi ni muhimu sana kuwa nazo kwenye kompyuta yako.?, kutoa jibu la swali hili leo tunakuletea programu kumi za muhimu kuwa nazo kwenye kompyuta yako hii haijalishi unatumia kompyuta ya aina gani iwe Windows au Mac programu hizi ni muhimu sana.
Kwa kuanza ni lazima ujue programu hizi zimegawanyika kutokana na matumizi hivyo kurahisisha kazi nitakuwekea matumizi ya programu hiyo ikifuatiwa na programu yenyewe, basi moja kwa moja twende tukaone programu hizi 10 muhimu kuwa nazo kwenye kompyuta yako.
- Ulinzi – Bitdefender
Ni hakika kwenye maisha yote ya binadamu kitu cha kwanza ni ulinzi na Afya, basi hata kwenye kompyuta yako ulinzi na Afya ya kompyuta yako ni kitu kikubwa sana na cha kwanza kabisa. Kuhakikisha hilo programu ya muhimu sana kuwa nayo kwenye kompyuta yako ni programu Anti virus ya Bitdefender, programu hii imeonekana kufanya vizuri sana kwa mwaka huu na yenye kutoa ulinzi wa hali ya juu sana kwenye kompyuta yako.
- Kisakuzi – Google Chrome
Katika swala zima la internet wote tunakubaliana kwamba Google ni kampuni ambayo imejiendeleza sana kwa upande huo, ukiacha kuwa kampuni hiyo ina miliki asilimia nyingi sana ya vitu vinavyo tegemewa mtandoni kama vile Google Search, Mfumo wa mzima Android, Play Store, Youtube pamoja na huduma nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikiwezesha huduma mbalimbali za mtandaoni hadi kumfikia mtumiaji. Sasa basi ili kukimbizana na kasi hii nakushauri kutumia Browser au kisakuzi cha Google Chrome kwani Google ndio baba wa internet na kwa kuwa karibu na google utaweza kupata kilicho bora zaidi.
- Mawasiliano – Mailbird
Mawasiliano kwenye kompyuta yako ni kitu cha msingi sana hapa nazumgumzia mawasiliano ya barua pepe kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia kompyuta zako kama sehemu ya mawasiliano basi programu ya Mailbird ni bora sana kuwa nayo. Hapa nasema programu hii badala programu kama Gmail ambazo zinatumiwa sana kwa sababu programu hii inakupa uwezo wa kutumia email zote yaani kama una email ya yahoo, gmail na hata zile nyinginezo za .com.
- Muziki na Video – VLC Media Player
Kama wewe umepanga kutumia kompyuta yako kwaajili ya kusikiliza na kucheza muziki na filamu basi ni lazima kuwa na programu ya VLC programu hii inakupa urahisi wa hali ya juu sana kucheza video zu filamu yoyote kwa haraka na kwa urahisi, hivyo sasa kama bado huna programu hii jua kwamba programu hii ni muhimu sana kuwa nayo.
- Kupakua Vitu Mbalimbali – Internet Download Manager
Kama wewe ni kijana na hata kama wewe n mtu mzima abisa lazima utakuwa umesikia au kuiona programu ya IDM hii ni programu muhimu sana kuwa nayo na ina rahisisha kabisa uwezekano wa mtumiaji kudownload vitu mbalimbali kutoka kwenye kompyuta, programu hii ni bora sana na inafanya kazi zaidi ya inavyotegemewa. Kama bado huna programu hii basi ni vyema kudownload sasa maana ni programu ya muhimu sana kuwa nayo kwenye kompyuta yako.
Download Internet Download Manager
- Programu Maalumu – Winzip
Kama umetumia kompyuta kwa muda mrefu lazima utakuwa umekutana na aina ya file linaloitwa (.zip) mafile haya yanaitaji programu maalum ya kufungua moja ya programu hizo ni programu inayojulikana kama Winzip, programu hii imekuwa kwa muda mrefu na imekuwa ikisaidia watu wengi sana ikiwa na uwezo wa kuweka password kwenye file bila kusumbuka kwa muda mrefu. Kama bado huna programu hii naomba ni kwambie kuwa kwa namna moja ama nyingine lazima utakutana na file za (.zip) hivyo ni vyema kuwa na programu hii ili kukupa urahisi wa kufungua file hilo unapokutana nalo.
- Uchapishaji – Microsoft Office
Wote tunajua matumizi ya MS Office programu hii inakusaidia kuwa na uwezo wa kuandika au kuchapa chochote kile kwa urahisi, lakini labda nikukumbushe umuhimu wa kuwa na programu hii na kama bado huna programu hii ni vyema ukaiweka kwenye kompyuta yako kwani nahakika lazima itakuja siku unataka kutumia programu hii.
- Kuamisha File – TeraCopy
Kama unataka kuongeza uwezo wa jinsi kompyuta yako inavyo hamisha mafile kutoka kifaa kimoja kupeleka kingine basi programu ya Teracopy ni muhimu sana kuwa nayo kwenye kompyuta yako, peogramu hii ni nmuhimu sana kuwa nayo kwenye kompyuta yako
- Ukarabati wa Kompyuta – CCleaner
Kama kompyuta yako imeanza kuwa slow na haifanyi baadhi ya vitu basi programu hii ni muhimu sana kuwa nayo. Na kama tunavyojua kuwa kutokana na matumizi ni lazima kwa namna moja ama nyingine kompyuta zetu ni lazima zitafika wakati zitakuwa slow hivyo ni muhimu kuwa na programu hii ya kukusaidia kutunza kompyuta yako pamoja na kufanya ukarabati wa Windows au MacOS pamoja na mafile yake.
- Kurudisha File Zilizofutika – MiniTool
Kama kwa namna moja ama nyingine umefuta kwa bahati mbaya baadhi ya file kwenye kompyuta yako basi programu hii ni muhimu sana kwenye kompyuta yako kwani zinakupa uwezo wa kurudisha file hizo moja kwa moja kwenye kompyuta yako. Kifupi kuwa na programu hii ni muhimu sana kwaajili ya tahadhari tena hasa kama kompyuta hiyo inatumiwa na mtu zaidi ya mmoja.
Na hizo ndio baadhi ya programu ambazo ni muhimu sana kuwa nazo kwenye kompyuta yako, kumbuka ni muhimu sana kuzingati kudownload programu hizo ili kuongeza afya pamoja na kudumu kwa kompyuta yako kwa muda mrefu.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.
Hizo programe unazidawnload Kwa kutumia file gan?
mim kompyuta yangu nikiweka video haziplay naomba mnisaidie.mimi mercy george 0627551730..