Kwa wale wasio ijua programu ya prisma, prisma ni programu maarufu ya kutengeneza katuni ambayo kwa mara ya kwanza ilikua ikipatikana kwenye iOS ikiwa ni moja kati ya programu zilizo fanya vizuri sana kwenye upande wa iOS kwa kupakuliwa zaidi ya mara milioni 10 programu hiyo imeonyesha kufanya vizuri sana kutokana na utoaji wa picha nzuri za katuni ambazo ni bora kuliko za programu nyingine.
Kwa kipindi kirefu sasa programu ya Prisma imekua ni moja kati ya programu ambazo zimekua zikiombwa sana na watumiaji wa mfumo wa Android hadi kufikia tarehe 24 July mwaka huu watengenezaji wa programu hiyo maarufu walitangaza rasmi kuachi programu hiyo kwenye vifaa na mfumo wa Android kwa ujumla.
Hadi kufikia leo tarehe 25 July programu hiyo imekwisha pakuliwa zaidi ya mara elfu 29,090 ikiwa ni masaa machache toka ilipoingia kwenye soko maarufu la Google Play Store, Hata hivyo watu wengi mbalimbali maarufu wameonekana wakifurahisha na kitendo cha programu hiyo kuingia kwenye mfumo huo wa Android.
Unaweza kupakua programu hiyo kwa kubofya hapo chini ili uanze kutengeneza katuni zako moja kwa moja kwenye simu yako ya Android.
Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.