Mpambano bado unaendelea, kampuni mbalimbali za kieletroniki zinaendelea kushindana kuonyesha teknolojia zake mpya kupitia mkutano wa CES 2019 na sasa tuko kwenye banda la kampuni ya Acer. Mara baada ya kuona laptop mpya ya Game kutoka kampuni ya Samsung hebu sasa hebu tuangalie laptop mpya ya Game ya Acer Predator Triton 900.
Acer Predator Triton 900 inakuja na kioo cha inch 17 ambacho kinakuja na teknolojia ya 4K pamoja na Touch Screen. Laptop hii inaendeshwa na processor ya core i7 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 16, Pamoja na Solid State Disk (SSD) ya TB 1. Vilevile Triton 900 inakuja na Graphics Card mpya na yenye nguvu kuliko zote ya RTX 2080 GPUs iliyozinduliwa hivi karibuni.
Muundo wa laptop hii hauna tofauti sana na ule wa laptop ya Samsung lakini utafauti upo kwenye laptop hii kwani inakuja na kioo chenye uwezo wa kuzunguka nyuzi 360, pia kioo hicho ni Touch Screen hivyo itakupa urahisi wa kukitumia hata kikiwa kimezunguka.
Kwa upande wa bei Predator Triton 900, inategemewa kuingia sokoni hivi karibuni ikiwa inauzwa bei sawa na IST kwa dollar za marekani $4,000 sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 9,203,000 bila kodi.
Laptop hii pia inakuja na toleo lingine la kawaida la Predator Triton 500 ambayo yenyewe inakuja na kioo cha inch 15 na bei yake itakuwa kuanzia dollar za marekani $1,800 sawa na Tsh 4,141,000 bila kodi. Sifa za laptop hii ni kama zilivyo kwenye jedwali hapo chini.
Kwa habari zaidi za teknolojia pamoja na yote yatakayojiri kwenye mkutano wa CES 2019 hakikisha unaendelea kuwa nasi tutakuletea yale yote ambayo ni muhimu wewe kuyajua kutoka kwenye mkutano huo ambao una anza rasmi hapo kesho huku Las Vegas nchini Marekani.