Baada ya Instagram kufanya majaribio ya uwezo mpya wa kupost picha au video zaidi ya moja kwenye post moja, sasa uwezo huo umekuja live kwenye programu zote za instagram. Mtumiaji ataweza kupost picha au video 10 kwa mara moja kwenye post moja ya mtandao huo wa Instagram.
Ili kupost picha nyingi kwa wakati mmoja uta bofya kitufe kipya kilichop upande wa kulia juu ya picha wakati unataka kupost kisha hapo utapata uwezo wa kuanza kupost picha 10 kwenye post moja. Kumbuka kuwa kwa sasa instagram imeweka uwezo wa kuweka maneno (caption) kwenye picha moja tu hivyo usitegemee kila picha itakuwa na maneno yake bali picha zote zitatumia (caption) moja.
Sehemu hiyo mpya tayari imeshanza kutoka kwa watu wote wenye programu za Instagram za iOS na Android hivyo pale unapona toleo jipya la programu hiyo ni vyema ukaupdate ili kuweza kupata sehemu hiyo mpya.
Kama unataka kuwa wakwanza kupata habari zote mpya za teknolojia kwa haraka hakikisha unadownload app ya Tanzania Tech na utapokea habari mpya kila siku, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.