Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5)

Kampuni ya Sony yazindua rasmi Playstation 5 hapo jana (Juni 11 2020)
Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5) Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5)

Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye hapo jana kampuni ya Sony ilizindua rasmi Playstation 5 (PS5) kupitia tamasha la mtandaoni.

Muonekano wa PlayStation 5

PS5 au Playstation 5 inakuja na muonekano wa tofauti huku ikiwa inakuja kwa matoleo mawili tofauti, toleo la kawaida (Standard edition) na toleo la kidigitali (Digital edition) toleo ambalo halina sehemu ya kuweka CD maarufu kama Optical drive.

Advertisement

Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5)

Playstation 5 inakuja na muundo wa kusimama huku ikiwa na kava jeupe kwa pembeni pamoja na rangi nyeusi kwa katika. Sehemu ya mbele ya PS5 inakuja na sehemu ya kuweka CD kwa toleo la kawada (Standard edition) pamoja na sehemu ya kuchomeka USB, taa ya Blue ya LED pamoja na sehemu za kupitisha hewa ambazo zipo kwa juu kwenye mkunjo. Kwa upande wa nyuma bado hakuna picha wala taarifa za muonekano wake.

Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5)

Kama unavyoweza kuona picha hapo juu, Playstation 5 ya kawaida (Standard edition) inakuja na muonekano ambao ni mpana zaidi, wakati PlayStation 5 (Digital edition) yenyewe inakuja na muonekano mwembamba zaidi na wakisasa.

Viunganisha vya PlayStation 5

Mbali na hayo, Playstation 5 inakuja na aina mpya kabisa za viendeshi (Controller) ambazo hazitumii waya (Wireless) na ambazo pia zinakuja na teknolojia mpya ya DualSense. Controller hizo pia zinakuja na haptic feedback pamoja na sehemu ya microphone ambayo imetengenezwa moja kwa moja kwenye viendeshi hivyo (built-in microphone).

Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5)

Mbali na hayo, Controller hizo zinakuja na kifaa maalum cha kuchaji controller hizo (DualSense Charging Station), kifaa ambacho kinaweza kuchaji controller zisizo zidi mbili.

Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5)

Pia kutakuwa na kamera maalum ambayo hiyo inayo teknolojia ya HD pamoja na headphone mpya zisizo tumia waya (Pulse 3D Wireless Headset), pamoja na kiendeshi au Media Remote ambayo inaweza kusaidia kutumia Playstation 5 kama kifaa cha media cha Blu-ray na streaming box.

Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5) Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5) Zifahamu Sifa, Muonekano, na Bei ya Playstation 5 (PS5)

Sifa za PlayStation 5

Kwa upande wa sifa za ndani, Playstation 5 inakuja na sifa zifuatazo

  • CPU: AMD Zen 2-based CPU with 8 cores at 3.5GHz (variable frequency)
  • GPU: 10.28 TFLOPs, 36 CUs at 2.23GHz (variable frequency)
  • GPU architecture: Custom RDNA 2
  • Memory interface: 16GB GDDR6 / 256-bit
  • Memory bandwidth: 448GB/s
  • Internal storage: Custom 825GB SSD
  • IO throughput: 5.5GB/s (raw), typical 8-9GB/s (compressed)
  • Expandable storage: NVMe SSD slot
  • External storage: USB HDD support (PS4 games only)
  • Optical drive: 4K UHD Blu-ray drive

Games Mpya za PlayStation 5

Mbali na hayo, Sony pia imezindua aina mpya za Game ambazo ni maalum kwa Playstation 5, game hizo ni pamoja na Marvel’s Spider-Man: Miles Morales, Horizon Forbidden West, Gran Turismo 7, Ratchet & Clank: Rift Apart, Resident Evil Village, NBA 2K21, Deathloop, Hitman III, na nyingine.

Pia kuna toleo jipya la game ya GTA V, toleo ambalo litakuja na muonekano bora pamoja na kuongezewa vitu zaidi. Toleo hilo la game ya GTA V linatarajiwa kutoka maalum kwa PS5 ikati ya nusu ya pili ya mwaka 2021. Unaweza kuona list nzima ya games hapa.

Bei ya PlayStation 5

Kwa upande wa bei, hadi sasa bado kampuni ya Sony haijatangaza rasmi bei ya Playstation 5, ingawa kuna tetesi ambazo zina onyesha bei ya PS5 inatarajiwa kuwa kati ya dollar za marekani $1000 au dollar za marekani $760, ambayo hiyo ni takribani zaidi ya shilingi za kitanzania TZS 2,316,000 au TZS 1,760,000 bila kodi.

Kumbuka bei hiyo inaweza kubadilika pale bei halisi ya PS5 itakapo tangazwa hivi karibuni. Kujua zaidi kuhusu upatikanaji wa Playstation 5 hapa nchini Tanzania, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use