Kwa sasa uwezo wa kucheza game za Play Station 3 katika kompyuta yako ni mkubwa sana kwani Sony imefanya rasmi kuwezekana kwa hatua hiyo. Hata hivyo game hizo zitakua zikichezeka kupitia Internet kwa kutumia huduma za (Sony’s streaming game service) ambazo zimepewa jina la PlayStation Now.
Hata hivyo huduma hiyo ya kutoka kwenye kampuni ya Sony inasemekana kuwepo takribani miaka miwili iliyopiata ambapo watumiaji alikua wakijisajili kwa viwango vya dollar $20 kwa mwezi na kwa miezi mitatu dollar $45, hata vivyo huduma hizi hupatikana kwenye baadh ya nchi kama vile USA, Canada pamoja na UK.
Ilikuweza kupata huduma hii kwa tanzania itakubidi kusubiri kidogo kwa huduma hii kufika nchini, ila kama unataka njia nyingine ya kucheza game hizo za Play Station 3 kwenye PC endelea kutembelea blog ya tanzania tech kwani tayari tumeshaweza kucheza game hizo kwenye pc sio siku nyingi tutarusha maelekezo hayo hapahapa kwenye blog ya tanzania tech, hakikisha hupitwi kwa kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech moja kwa moja kwenye simu yako ya Android pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.