Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Aina Nne za Plastiki Ambazo Hutakiwi Kutumia Mara Mbili

Hizi ndio siri zilizoko chini ya vifaa vya plastiki soma kuzijua sasa…
plastiki plastiki

Wote tunatumia vifaa vya plastiki na kati yetu plastiki pia ni sehemu muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku, hivyo basi ni vyema leo kujua siri ambazo ulikua hujui zilizoko chini ya vifaa vya plastik.

Ukweli ni kwamba kila plastiki unayo iona imetengenezwa kwa aina tofauti ya plastiki, aina hizo zimetengenezwa maalum ili kudhibiti ubora wa kitu kilichopo ndani ya plastiki au wakati mwingine zinatengenezwa hivyo ili kuwezesha matumizi bora ya kifaa hicho.. hivyo basi zifuatazo ni aina za plastiki ambazo hutakiwi kutumia mara mbili.

Advertisement

Maelezo zaidi ni kuwa, ni muhimu kuwa makini unapotumia plastiki ni bora kuwa makini kwa kuangalia aina ya alama ambazo zinapatikana chini ya plastiki ili kujua kama unaweza kutumia plastiki hiyo kwa mara ya pili.

Ni vyema kuwa makini na chupa au vyombo vya plastiki vyenye alama za pembe tatu na maandishi ya V kisha 3 kwenye pembe tatu, PS kisha 6 kwenye pembe tatu, pamoja na OTHER kisha 7 kwenye pembe tatu kwani vyombo hivi havifai kwa matumizi ya kuweka vyakula au maji, lakini pia kumbuka chupa au vyombo vya plastiki vyenye alama za PETE kisha 1 kwenye pembe kwani hivi inaruhusiwa kutumika mara moja na sio zaidi kwani vyombo hivi vikipata Oxygen au vikipigwa na jua kwa muda huweza kutoa kemikali zinazoweza kuadhiri afya yako.

Kwa matumizi salama ya vyombo vya plastiki ni vyema kuangalia vyombo vyenye alama za HDPE kisha 2 kwenye pembe tatu, LDPE kisha 4 kwenye pembe tatu, pamoja na PP kisha 5 kwenye pembe tatu, vifaa hivi ni salama kabisa kwa kutumia mara zaidi ya moja lakini kumbuka ni vyema uwe unaviosha kwa umakini na kwa kutumia sabuni maalum.

Najua imekaa ki Afya zaidi lakini nimeona ni bora nikufahamishe hii kwani aina hizi za plastiki ndizo tunazo tumia kila siku hivyo nimeona ni muhimu sana wewe kuweza kujua hili ili kuweza kujilinda kwani wengi wetu hatuna ustarabu wa kuangalia alama hizi pale tunapo nunua vifaa au vyombo hivi tena hasa vile ambavyo tunatumia kwa matumizi ya kula ama kunywa.. Hope this help!!

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Eartheasy Blog

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use