WhatsApp imekuwa ikiongeza sehemu mpya kila baada ya muda maalum, hivi karibuni mabadiliko ya sera za faragha yameleta wasiwasi baina ya watumiaji wa programu hiyo na kusababisha baadhi ya watumiaji kuhama kwenye programu hiyo na kuanza kutumia programu ya Telegram.
Pamoja na hayo WhatsApp imekuwa ikituma ujumbe wa maelekezo ya sera hizo mpya za faragha kupitia sehemu ya Stories ili kutoa ufahamu zaidi kuhusu sera hizo mpya na umuhimu wa kukubali vigezo hivyo vipya.
Lakini mbali na hayo ambayo hadi sasa yanaendelea kuzua taharuki kwa watumiaji wa programu hiyo, pengine habari hii mpya inaweza kufanya watumiaji wengi kufikiria kukubali sera hizo na kuendelea kutumia programu ya WhatsApp.
Kwa mujibu wa tovuti ya Wabetainfo, programu ya WhatsApp inatarajiwa kuongezewa sehemu mpya ambayo itasaidia watumiaji kuweza kutuma picha ambazo zinajifuta zenyewe mara baada ya aliyetumiwa kuzifungua na kufunguka chati husika.
Pia kupitia sehemu hiyo watumiaji hawata ruhisiwa kuhifadhi picha hiyo kwenye simu kwa namna yoyote. Kwa mujibu wa picha hizo, inaonekana kutakuwa na kitufe kipya ambacho kitaruhusu watumiaji kushiriki picha ambazo hujifuta, na mtumiaji anapo pokea anatakiwa kubofya picha hiyo ili kuweza kuona picha yenyewe.
Mara baada ya mtumiaji kufunga ujumbe huo moja kwa moja ataweza kuangalia picha uliyotumiwa na baada ya kufunga picha hiyo moja kwa moja picha hiyo iyajifuta kwenye chats zako na utaweza kuiona tena
Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi sehemu hii itakuja lini, kama unataka kujua zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku kupata taarifa zaidi kuhusu sehemu hiyo na nyingine nyingi kwenye programu mbalimbali.