Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Picha za Muonekano wa Simu Mpya za Tecno Spark 2

Inasemekana kuwa hizi hapa ndio picha halisi za Simu hizi Mpya
Picha za Tecno Sparks 2 Picha za Tecno Sparks 2

Hivi karibuni tulitoa ripoti kuhusu kampuni ya Tecno kujiandaa na uzinduzi wa simu mpya za Tecno Spark 2, muda mchache umepita wakati bado tukitegemea simu hizo kuzinduliwa mwezi huu, tayari kumesha vuja picha ambazo inasemekana ndio muonekano halisi wa simu hizo mpya za Tecno Spark 2.

Wakati bado hakuna taarifa za uhakika zaidi kuhusu picha hizo kama ndio muonekano halisi wa simu hizo, lakini uhakika kuwa kampuni ya Tecno inafikiria kuingiza toleo jipya la simu hizo mpya za Tecno Spark ndani ya mwezi huu wa sita.

Advertisement

Kama nilivyo sema hapo hawali bado hakuna uhakika kama huu ndio muonekano halisi wa simu hizo za Tecno Spark 2, lakini kama ndio muonekano halisi wa simu hizo basi kampuni ya Tecno kwa mara nyingine tena imepiga hatua kwa kutengeneza muonekano mzuri kwenye simu zake hasa za mwaka huu 2018.

Kwa mujibu wa tetesi kutoka tovuti mbalimbali, Tecno Spark 2 inatarajiwa kuja kwa matoleo mawili, kiwa ni pamoja na toleo la Tecno Spark 2 pamoja na Spark 2 Plus. Toleo la Tecno Spark 2 inasemekana kuwa itakuwa ni simu inayotumia mfumo wa Android Go, na Tecno Spark 2 Plus yenyewe itakuwa inatumia mfumo wa kawaida wa Android Oreo 8.0 au Android 8.1, Hata hivyo kwa mujibu wa tetesi hizo zifuatazo ndio sifa za awali za simu hizi.

Sifa za Awali za Tecno Spark 2 (Go Edition)

  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo (Android Go Edition)
  • Kioo –  6.0 inches (~78.2% screen-to-body ratio) Screen Touch, 1440 x 720 pixels, 18:9 ratio (~274 ppi density)
  • Uwezo wa Processor – quad-core 1.3 GHz ARM Cortex-A7 MediaTek Mt6580 chipset
  • Uwezo wa Graphics – Mali-400MP2
  • Ukubwa wa Ndani na RAM – 16GB, 1GB RAM
  • Kamera ya Nyuma – 13MP, f/2.0, autofocus, quad-LED flash
  • Kamera ya Mbele – 8 MP, f/2.4 dual-LED flash
  • Mengineyo – GSM / HSDPA, Fingerprint Scanner, Accelerometer, gyro, barometer, v4.0, A2DP
  • Uwezo wa Battery – Non-removable Li-Ion 3500 mAh battery
  • Rangi – Champagne Gold, Choral Blue, Metal Silver and Phantom Black

Update : Tayari simu mpya ya Tecno spark 2 imesha zinduliwa rasmi, soma hapa kujua sifa kamili za simu hii pamoja na bei yake kwa hapa Tanzania.

Sifa za Awali za Tecno Spark 2 Plus

  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo
  • Kioo –  6.0 inches (~78.2% screen-to-body ratio) Screen Touch, 1440 x 720 pixels, 18:9 ratio (~274 ppi density)
  • Uwezo wa Processor – quad-core 1.3 GHz ARM Cortex-A7 MediaTek Mt6580 chipset
  • Uwezo wa Graphics – Mali-400MP2
  • Ukubwa wa Ndani na RAM – 16GB, 2GB RAM
  • Kamera ya Nyuma – 13MP, f/2.0, autofocus, quad-LED flash
  • Kamera ya Mbele – 8 MP, f/2.4 dual-LED flash
  • Mengineyo – GSM / HSDPA, Fingerprint Scanner, Accelerometer, gyro, barometer, v4.0, A2DP
  • Uwezo wa Battery – Non-removable Li-Ion 3500 mAh battery
  • Rangi – Champagne Gold, Choral Blue, Metal Silver and Phantom Black

Kwa sasa bado hakuna taarifa kamili ni tarehe gani simu hizi zitazinduliwa, ila kwa mujibu wa tetesi hizi huenda simu hizi zikazinduliwa katikati ya mwezi huu wa sita au mwishoni mwa mwezi huu. Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use