Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hii Ndio Picha Yenye Likes Nyingi Kuliko Zote Instagram (2019)

Picha ya Yai imeipita picha ya Mtoto wa Kylie Jenner kwa kuwa na Likes nyingi zaidi
picha yenye likes nyingi instagram 2019 picha yenye likes nyingi instagram 2019

Kylie Jenner ni jina linalo kuja kama ukitafuta list ya watu maarufu wanaolipwa pesa nyingi kupost tangaza kwenye akaunti zao za Instagram. Lakini pia siku za nyuma, picha ya mtoto wa Kylie Jenner ndio ilikuwa picha inayopendwa zaidi au yenye like nyingi kwenye mtandao wa Instagram kwa kuwa na likes zaidi ya milioni 18.2.

Picha yenye like nyingi instagram 2018

Advertisement

Well kwa sababu huu ni mwaka 2019 na mambo yanabadilika, siku mbili zilizopita picha ya mtoto wa Kylie Jenner imeshuka na sio picha yenye like nyingi kupita zote kwenye mtandao wa Instagram.

Kwa sasa rekodi hiyo imeshikiliwa na akaunti ya EGG GANG, ambayo picha pekee ya yai iliyoko kwenye akaunti hiyo ndio picha iliyoshikilia rekodi ya kuwa picha inayo pendwa zaidi duniani au yenye likes nyingi zaidi, huku ikiwa na likes zaidi ya milioni 47.3 hadi sasa.

Hii Ndio Picha Yenye Likes Nyingi Kuliko Zote Instagram (2019)

Picha hii inaingia kwenye rekodi hii ya dunia, na kwa mara ya kwanza hii ndio picha ambayo haina mtu kuweza kushikilia rekodi hii. Picha zote ambazo zimewahi kushikilia rekodi hii zinasemekana zote zilikuwa ni picha za watu maarufu duniani.

Kama unavyoweza kusoma Caption ya post hiyo, mwenye akaunti hiyo (EGG GANG) alitengeneza akaunti hiyo maalum kabisa kwaajili ya kuishinda rekodi iliyoshikiliwa na Kylie Jenner February mwaka 2018, ilipo kuwa picha yenye likes nyingi kuliko zote kwenye mtandao wa Instagram.

Kwa sasa bado haijajulikana wazi faida ya kushikilia rekodi hii, ila ukiangalia Follower kwenye akaunti hiyo ni zaidi ya milioni 2.2 pengine kutokana na muonekano wa akaunti hiyo inaweza kuwa akaunti ya biashara kwa ajili ya matangazo hasa kwa makampuni makubwa yanayo jihusisha na biashara ya mayai nchini marekani, kama vile kampuni ya Cal-Maine ambayo ndio kampuni kubwa ya uzalishaji wa mayai nchini marekani, huku ikisemekana kuhudumia mayai kwa zaidi ya robo ya wananchi wa marekani.

Anyway, kwa sababu mwaka 2019 bado ni mchanga, pengine picha hii inaweza kuja kupitwa na picha nyingine siku za karibuni. Lakini kama wewe ni mpenzi wa Je wajua na unapenda kujua, basi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kwani tutakupa taarifa tu pale picha nyingine itakapo fanikiwa kushilia rekodi ya picha yenye likes nyingi zaidi kwenye mtandao wa Instagram.

Makala imeongezwa kuonyesha idadi ya likes hadi leo tarehe 17 ya mwezi January mwaka 2019

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use