Tayari ni mwezi wa pili wa mwaka 2019 na siku chache zimebaki hadi kuzinduliwa rasmi kwa simu mpya ya Samsung Galaxy S10. Kama unavyojua, kadri muda unavyozidi kuwa mchache ndivyo habari zaidi za simu hii zinavyozidi kujulikana zaidi.
Hivi karibuni kumevuja picha ambayo inasemekana ndio picha halisi yenye kuonyesha muonekano wa Simu mpya ya Galaxy S10+. Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, picha hii ambayo imetolewa na 91 Mobiles inaonyesha simu hiyo ikiwa na kamera tatu kwa nyuma, pamoja na kamera mbili kwa mbele kama ilivyotajwa hapo awali kwenye tetesi mbalimbali za simu hii.
Kama unavyo wenza kuona kwenye picha hapo juu, Galaxy S10 Plus inatarajiwa kuja na kioo kikubwa ambacho kinasemekana kuja na teknolojia ya QHD na Super AMOLED Display. Mbali na hayo kama umegundua kwenye picha hiyo simu hiyo inaonekana kutokuwa na sehemu ya fingerprint, hii ina maana kuwa sehemu ya fingerprint itakuwa juu ya kioo au inaweza ikawa pembeni au inaweza kuwa haipo kabisa na huwenda galaxy S10 Plus ikiwa inatumia zaidi ulinzi wa Iris Scanner.
https://tanzaniatech.one/finder/comparison/samsung-galaxy-s10-vs-samsung-galaxy-s10-plus/
Mbali na hayo pia imevuja video ambayo inaonyesha simu mpya inayojikunja ya Samsung Galaxy F. Kwenye video hiyo Galaxy F inaonekana kwa muda mfupi sana hivyo kama hutoweza kuona simu hiyo inabidi kurudia tena kuangalia kwa makini hasa sekunde ya 0:23 ya kwenye video hiyo hapo chini.
Kama unavyoweza kuona video hiyo ni ishara kuwa Samsung iko mbioni kuzindua simu hiyo inayo jikunja hivyo pengine tutegemee kuiona simu hiyo hivi karibuni inawezekana hata kwenye mkutano wa MWC 2019.