Siku za karibuni tumesikia tetesi mbalimbali kuhusu simu mpya ya Galaxy Note 8 ambayo kwa mujibu wa tovuti ya techradar simu hiyo imapagwa kutoka mwezi wa nane tarehe 23 huko nchini marekani.
Lakini wakati tukisubiri tarehe ya kutoka kwa simu hiyo bado tetesi nazo zimezidi kuwa nyingi sana, lakini pamoja na tetesi hizo kuwa nyingi tetesi hii ninayo kusogezea leo imenifanya kwa kiasi kikubwa kutaka kusikia maoni yako pindi utakapo weza kuona picha hii.
Ukweli ni kuwa tumesha ona picha nyingi sana za mifano ya simu hiyo ambayo bado haijatoka, lakini mfano huu au picha hii ndio ya kwanza yenye muonekano huu ambao pengine ndio ukawa wa simu hiyo ambayo tunaitarajia mwezi wa nane, Hivyo basi hebu niambie wewe unaonaje je unadhani pengine picha hii ndio muonekano halisi wa simu hiyo mpya kutoka Samsung yaani Galaxy Note 8.?
Je huu ndio muonekano halisi wa Samsung Galaxy Note 8..? pic.twitter.com/a0wRs11XmH
— Tanzania Tech (@tanzaniatech) July 16, 2017
Kwa upande wangu ukiniuliza swali hilo basi naweza nikakwambia kwa namna moja ama nyingine inawezekana kabisa picha ya simu hii ndio ikawa ndio picha ya Galaxy Note 8, moja ya sababu zangu za kusema hivyo ni pamoja na ….
Hivi karibuni kwenye ukurasa wa Twitter wa Samsung Exynos ambao unatangaza processor zinazotumiwa na samsung kulitokea picha ambayo ina fanana sana na picha hiyo hapo juu, picha hiyo ambayo pengine iliweka na Samsung ili kusema kuwa simu hiyo (Note 8) itakuja ikitumia processor hizo maarufu za Exynos 9, na hii ndio picha yenyewe..
Ukijaribu kuangalia picha hii utagundua kuwa hakuna simu yoyote ambayo ina muundo huu ambayo tayari imesha toka na pia ukiangalia karibu zaidi utaona muundo wa simu hii ni sawa kabisa na muundo ambao Samsung wamekua wakitumia kwenye simu zake za Note tofauti ni kuwa sasa kioo kimeongezwa kwa kutolewa kingo za juu na chini.
Hebu niambie wewe unaonaje kwenye picha hizo mbili je unadhani huu ndio muonekano wa halisi wa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 8 na kama ndio je ungependa kununua simu yenye muundo na muonekano huu, tujulishe kupitia maoni yako hapo chini.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.
Chanzo : Techradar