WhatsApp imekuwa ni moja kati ya nyenzo muhimu sana kwa mawasiliano siku hizi, wengi wetu hutumia progamu hii kwa biashara, na wengine hutumia kwa kuwasiliana na ndugu na jamaa wa karibu.
Kuliona hili WhatsApp imekuwa ileta maboresho mbalimbali ambayo husaidia watu kuweza kuwasiliana kupitia programu hiyo kwa urahisi, hivi karibu sehemu mpya kwenye programu hiyo ni pamoja na sehemu ya kutuma picha ambayo itaonekana mara moja tu.
Tuma Picha Inayo Onekana Mara Moja WhatsApp
Kwa mujibu wa WhatsApp sehemu hii inategemewa kuanza kupatina hivi karibuni ambao utaweza kutuma picha ambayo ikimfikia mlengwa ataweza kuangalia picha hiyo mara moja tu na baada ya kufunga picha hiyo basi picha hiyo itaweza kupotea moja kwa moja.
Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu, ili kutuma picha inayoweza kuangaliwa mara moja unatakiwa kubofya sehemu ya kamera kwenye uwanja wa meseji.
Kisha moja kwa moja piga picha na endelea kwa kubofya kitufe cha alama ya 1 yenye duara na endelea kwenye hatua inayo fuatia.
Baada ya kubofya sehemu hiyo kama ni mara yako ya kwanza kutumia sehemu hii utaweza kuona maelezo ya kukaribisha kutumia sehemu hii bofya ok na endelea kwa kutuma picha yako.
Baada ya kutuma picha au video moja kwa moja utaweza kuona maandishi yanayo ashiria kilichomo ndani, watu wote anaetuma na anaepokea awatoweza kuona preview ya picha au video isipokuwa neno “video” au “photo” kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.
Baada ya mpokeaji kuweza kuangalia picha au video aliyo tumiwa, moja kwa moja aliye tuma picha hiyo ataweza kuona maneno “video” au “photo” yakibadilika na kuwa “opened” hii ikiwa ishara kwa picha au video uliyotuma imesha angaliwa na mpokeaji.
Kwa kufuata hatua hizo moja kwa moja utaweza kutuma picha au video Inayoweza kuonekana mara moja ndani ya programu ya WhatsApp. Kumbuka unatakiwa ku-update programu yako ya WhatsApp kabla ya kuona sehemu hii, pia picha isipo funguliwa kwa muda mrefu itapotea au itakuwa expired na hakuna mtu ambaye ataweza kuiona tena.