Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Photo Scan Programu Mpya Kutoka Google Kwaajili ya Picha

Geuza picha za kwenye album yako kuwa za digital kwa kutumia Photoscan kutoka kampuni ya Google
Photo Scan Photo Scan

Kama tunavyojua Google ni moja kati ya kampuni za sasa zinazo ongoza sana katika swala zima la ubunifu wa programu mbalimbali, ndio maana hivi karibuni kampuni hiyo imezundia programu mpya ya Photo Scan maalumu kwaajili ya kufanya picha zako za kwenye album yako ya karatasi kuwa kwenye mfumo wa digitali.

Jinsi programu hiyo inavyofanya kazi, utatakiwa kuwasha programu hiyo kisha itawasha kamera ya simu yako moja kwa moja kwa kuanza kuscan picha zako. Baada ya hapo kwenye kioo cha simu yako uaona vidoti vinne ambavyo utatakiwa kufuata kisha shikilia simu yako kwenye eneo hilo mpaka doti hilo litakapo jaa, fanya hatua hizo kwa kila doti mpaka vidoti vyote vinne vikamilike. Ukisha maliza hapo picha yako itakua tayari ikiwa na rangi bora pamoja na uhalisia wa picha ya kamera ya simu.

Advertisement

Programu hiyo ya Photo Scan inahifadhi picha zako kwenye programu ya Google Photos ambayo inakuja na simu yako ya Android na pia Programu ya Photo Scan kwa sasa ipo tayari kwenye Masoko (store) yote ya mifumo yote ya Android pamoja na iOS, unaweza kudownload Programu hiyo hapo chini.

PhotoScan by Google Photos – Android

PhotoScan by Google Photos – iOS

Programu hii imekuja pamoja na update za programu ya Google Photos ambayo inakupa uwezo wa kuedit picha pamoja na kutengeneza video fupi. Kama umeona update za programu hiyo hakikisha unadownload ili uweze kuona utofauti wa programu hiyo bora ya kuhifadhi picha.

Ili kupata habari zote za teknolojia kila siku endelea kutembelea Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use